June 14, 2014

Mwigizaji Harrison Ford apata ajali akirekodi filamu.

Mcheza filamu mkongwe wa nchini Marekani Harrison Ford anapatiwa matibabu hospitalini kutokana na majeraha aliyopata wakati akirekodi f... thumbnail 1 summary
Harrison Ford
Mcheza filamu mkongwe wa nchini Marekani Harrison Ford anapatiwa matibabu hospitalini kutokana na majeraha aliyopata wakati akirekodi filamu yake mpya inayokwenda kwa jina la Star
Wars.
Harrison Ford mwenye umri wa miaka 71 amevunjika kifundo chake cha mguu baada ya
mlango wa eneo la kutengeneza magari kumuangukia wakati wakirekodi filamu katika studio za Pinewood nchini Marekani.
HarrisonFordHanSolo
Mwigizaji huyo wa Hollywood ambaye ameigiza katika filamu ya Star Wars ambapo sasa anarekodi
sehemu ya saba ya mwendelezo wa filamu hiyo alikimbizwa hospitalini ambapo msemaji wa kampuni ya kutengeneza filamu amesema wataendelea kurekodi kama kawaida.
Filamu hiyo inaigizwa na wasanii wenginge wakubwa kama Lupita Nyong’o, John Boyega, Daisy Ridley, Adam Driver, Oscar Isaac, Andy Serkis, Domhnall Gleeson, na Max von Sydow.
Tukio hilo limetokea wakati wa mwendelezo wa sehemu ya saba ya war Stars ambayo inatarajia kukamilika hivi karibuni.

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW: