December 23, 2016

Jay Moe anavyokula sahani moja na kizazi cha ‘dab’

Juma ‘Jay Moe’ Mchopanga aka Mbakiaji, ni rapper mkongwe ambaye kama ng’ombe mzee, hazeeki maini. Kwa takriban miaka 15 ya career yake, Jay... thumbnail 1 summary
Juma ‘Jay Moe’ Mchopanga aka Mbakiaji, ni rapper mkongwe ambaye kama ng’ombe mzee, hazeeki maini. Kwa takriban miaka 15 ya career yake, Jay Moe hajawahi kuonekana kuhangaika kuonesha ujuzi wake kwenye hip hop.


Ni miongoni mwa wasanii wa zamani wenye hits nyingi ambazo licha ya kuwa na muda mrefu tangu zitoke, bado zinaweza kusikika na upya masikioni mwako. Nyimbo kama Bishoo, Mvua na Jua, Kama Unataka Demu, Maisha ya Boarding, Story 3, Famous ni miongoni mwa nyimbo zake classic zilizompa heshima. Huwezi kusahau hits zingine alizoshirikishwa kama Zeze ya TID, Kimya Kimya aliyofanya na marehemu Ngwair au Jirushe ya Ferooz.

Pamoja na ukongwe huo, Jay Moe amethibitisha mwaka huu kuwa anaweza kuwa rapper hatari katika kizazi cha trap na dab. Aliamua kuchukua risk iliyozaa matunda, kufanya muziki ambao rappers wenye heshima kama yeye wanaogopa kuufanya kwa kile wanachoamini wataonekana wanatapatapa. Wimbo wake Pesa ya Madafu ulimhamisha kutoka kwenye rap yake iliyozoeleka, hadi katika rap ya vijana wa leo, rap ya kizazi cha dab.


Jay Moe anasema aliamua kubadilika kiasi hicho kutokana na kukosolewa na watu kadhaa kwenye wimbo kabla ya huo, Hili Game ambao anasema alifanya makusudi kwa kuogopa kuja na ladha mpya kufuatia ukimya wake wa muda mrefu.
Anasema hiyo ilimpa sababu ya kuja na wimbo wenye usasa mwingi kwakuwa ni nyimbo ambazo anasikiliza pia. “Huko nyuma sikuwa na wimbo ambao ungeweza kuconnect watu wa jinsia tofauti na umri tofauti,” rapper huyo alikiambia kipindi cha Ngaz Kwa Ngaz cha Salama Jabir miezi kadhaa iliyopita.
“Kwasababu umekuwa ni wimbo ambao hata watoto wadogo nikipita tu wanaimba ‘pesa ya madafu.’
Na kiukweli kubadilika kwa Jay Moe kumekuwa na mafanikio makubwa kwasababu Pesa ya Madafu haikosi kwenye orodha ya nyimbo 10 za hip hop zilizotamba zaidi kwenye redio na TV mwaka huu.
Kubadilika kwake pia, kulikuwa na sababu za kiuchumi na kugoma kuendelea kushikilia misingi ya hip hop ambayo haina faida.
“Leo wakitajwa wasanii wakali wa hip hop hata watano Jay Moe atatajwa lakini wakitajwa wasanii watano wa hip hop wenye mafanikio Jay Moe hayupo,” alisema kwenye interview moja.
“Kwanini na mimi nisiwe kama Nay wa Mitego, kwanini mimi nisiwe kama AY na Profesa Jay wakati kipaji changu kinafaa niwe hivyo, zaidi ya hivyo. Wasanii wengi wa hip hop wanataka ku-maintain culture ambayo haipo tena. Wote tunakubali kuwa sasa hivi muziki biashara kwahiyo tukubali kufanya ule wa kibiashara ambao hatutokuwa na malalamiko ‘wasanii wa zamani tunabaniwa kwenye media’ sio kweli ni kwasababu hatujapeleka content ambayo media na wasikilizaji wanaitaka,” alisisitiza rapper huyo.
Jay Moe hajaishia kwenye Pesa ya Madafu, bali amekuja kuonesha kuwa amekimudu vizuri kizazi cha trap na dab kwenye wimbo alioshirikishwa na Songa – rapper mwingine aliyeamua kubadilisha muelekeo.
Mwendo Tu, ni wimbo mwingine wa trap ambao kutokana na ulivyo, umewaongezea wigo wa mashabiki hasa ‘teenagers’ na wasichana ambao haikuwa rahisi kuwapata kwa nyimbo walizokuwa wamezoea kufanya.
Nguvu ya wimbo huo imeongezeka zaidi kutokana na kuwa na video kali inayovutia macho ya kila mpenda vitu vizuri. Kwa mabadiliko hayo ya Jay Moe, ni wazi kuwa ana miaka mingi kwenye game na rappers wengi wapya watakuja na kuondoka na kumwacha akipeta kama na wao watashindwa kuwa vinyonga.

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW:

Picha: Carlos Tevez afunga ndoa na mpenzi wake wa tangu utotoni

Mshambuliaji wa zamani wa vilabu vya Manchester United na City, Carlos Tevez hatimaye amefunga ndoo na mpenzi wake wa tangu utotoni, ... thumbnail 1 summary


Mshambuliaji wa zamani wa vilabu vya Manchester United na City, Carlos Tevez hatimaye amefunga ndoo na mpenzi wake wa tangu utotoni, Vanesa Mansilla, mjini San Isidro

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW:

So which celebs had the biggest birthdays this year?

Sharing happiness is exciting, especially for our celebrities. We mark the biggest birthdays that our celebs had this year. thumbnail 1 summary


Sharing happiness is exciting, especially for our celebrities. We mark the biggest birthdays that our celebs had this year.

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW:

Celine Dion apiga chini ofa ya Donald Trump

Muimbaji mkongwe wa nyimbo za taratibu kutoka Canada, Celine Dion ameongeza idadi ya wasanii waliopiga chini ofa ya kutumbuiza kwenye s... thumbnail 1 summary

Muimbaji mkongwe wa nyimbo za taratibu kutoka Canada, Celine Dion ameongeza idadi ya wasanii waliopiga chini ofa ya kutumbuiza kwenye sherehe za kuapishwa kwa Rais mteule wa Marekani Donald Trump.

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW:

Jeshi la Polisi latoa onyo msimu wa sikukuu

Jeshi la polisi nchini limetoa onyo kali kwa wananchi waliojipanga kufanya uhalifu katika kipindi cha kuelekea sikukuu za mwisho wa m... thumbnail 1 summary


Jeshi la polisi nchini limetoa onyo kali kwa wananchi waliojipanga kufanya uhalifu katika kipindi cha kuelekea sikukuu za mwisho wa mwaka.

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW:

Gigy Money aeleza jinsi alivyopambana kumpata mpenzi wake mpya Mo J – Part 2

Video vixen ambaye pia ni mtangazaji wa Choice FM, Gigy Money ameendelea kufunguka mbele ya Bongo5TV kueleza namna ambavyo alitumia nguvu... thumbnail 1 summary
Video vixen ambaye pia ni mtangazaji wa Choice FM, Gigy Money ameendelea kufunguka mbele ya Bongo5TV kueleza namna ambavyo alitumia nguvu nyingi kumpata mpenzi wake ambaye anafanya naye kipindi kimoja cha redio, Choice FM.

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW:

Dereva bodaboda akatwa sikio kwa tuhuma ya kufumaniwa na mke wa dereva teksi

Dereva bodaboda wa Mji Mdogo wa Qatesh wilayani Hanang’ Mkoa wa Manyara, amekatwa sikio kwa kisu kwa tuhuma za kufumaniwa akiwa na ... thumbnail 1 summary


Dereva bodaboda wa Mji Mdogo wa Qatesh wilayani Hanang’ Mkoa wa Manyara, amekatwa sikio kwa kisu kwa tuhuma za kufumaniwa akiwa na mke wa dereva wa teksi.

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW:

Orodha ya Fifa: Argentina bado yaongoza Tanzania ya panda

Shirikisho la soka Duniani FIFA December 22 2016 limetoa orodha mpya ya viwango vya soka, Tanzania imefanikiwa kupanda katika viwango... thumbnail 1 summary


Shirikisho la soka Duniani FIFA December 22 2016 limetoa orodha mpya ya viwango vya soka, Tanzania imefanikiwa kupanda katika viwango hivyo vya soka vya FIFA.

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW:

Polisi waliomdhalilisha mchungaji wakufuzwa kazi

Askari polisi wanne mkoani Kilimanjaro waliotuhumiwa kutengeneza tukio la ushoga kwa mchungaji wa kanisa la kiinjili la kilutheri Tan... thumbnail 1 summary


Askari polisi wanne mkoani Kilimanjaro waliotuhumiwa kutengeneza tukio la ushoga kwa mchungaji wa kanisa la kiinjili la kilutheri Tanzania(KKKT) wamefukuzwa kazi.

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW:

Vanessa Mdee adai ataachia wimbo wake na Barnaba mwakani

Vanessa Mdee amethibitisha kufanya wimbo mwingine na Barnaba ambao utatoka mwakani. thumbnail 1 summary


Vanessa Mdee amethibitisha kufanya wimbo mwingine na Barnaba ambao utatoka mwakani.

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW:

Mambo ya shemeji zima taa yatokea kariakoo, shuhudia Fumanizi hili live hapa

MFANYABIASHARA maarufu wa simu za mikononi maeneo ya Kariakoo jijini Dar, aliyefahamika kwa jina moja la Devi, hivi karibuni alipatwa na so... thumbnail 1 summary
MFANYABIASHARA maarufu wa simu za mikononi maeneo ya Kariakoo jijini Dar, aliyefahamika kwa jina moja la Devi, hivi karibuni alipatwa na soni ya aina yake baada ya kukutwa katika nyumba ya kulala wageni akiwa na mke wa rafiki yake wa karibu.

Mtoa habari makini aliliambia gazeti hili kuwa kisa kizima kilianza baada ya mwenye mali (mume) kukuta ujumbe mfupi wa simu katika kilongalonga cha mkewe unaoashiria mambo ya mapenzi na mbaya zaidi, meseji hiyo ilitoka kwa rafiki yake huyo.

Licha ya kukuta ujumbe huo wa kimahaba, chanzo chetu kilidai kuwa pia mume huyo alikutana na sms kadhaa zilizokuwa zimetuma fedha kwa njia ya mtandao wa simu, zikielekezwa kwa dada huyo kwa ajili ya matumizi yake.

Baada ya jamaa huyo kujiridhisha kuwa Davi alikuwa na nia mbaya na mkewe, mume huyo aliamua kuanzisha mkakati na kumtuma mdogo wake kufuatilia ishu nzima kwani yeye alibanwa na majukumu mengine ya kikazi.

Bila kujua kuwa nyendo zao zinafuatiliwa, Davi na shemeji yake walipanga kukutana katika hoteli moja (jina linahifadhiwa)iliyopo Sinza na baada ya kupata chumba na kuingia ndani, bila hofu, walianza kujiandaa kwa ajili usaliti.

Huku mwanaume akiwa ameshatoa nguo zake sambamba na mpenzi wake, mlango wa chumba chao uligongwa, lakini wakiwa hawana hofu,wakiamini ni mhudumu walifungua na wote kupatwa na bumbuazi baada ya kugundua aliyekuwa mbele yao ni mdogo wa mwenye mke ambaye wote wanamfahamu!

“Huwezi kuamini, baada ya sisi kuingia chumbani na kuwakuta kama walivyozaliwa, jamaa alikimbilia chooni na kwa jinsi alivyokuwa, alionyesha kabisa kuhitaji kujitumbukiza, lakini bahati nzuri vyoo vile ni vya kisasa,” kilidai chanzo hicho.

Mwandishi wetu alimtafuta kwa njia ya simu mwenye mke kutaka kujua kilichoendelea baada ya tukio hilo ambapo alipopatikana alisema:

“Ni kweli tukio hilo limetokea ila siwezi kuzungumzia zaidi, jamaa alikuwa akinizunguka kwa mke wangu lakini arobaini yake imefika, zaidi nenda Kituo cha Polisi Oysterbay utaelezwa kila kitu.”
GPL

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW:

HUU Wimbo Mpya wa Baghdad na Roma f/ Snura Unaitwa K Utata Mtupu Mwanzo Mwisho...Usikilize Hapa

Baghdad na Roma wameigeukia Singeli katika wimbo wao K waliomshirikisha Snura. Ni wimbo utakaokuvunja mbavu kwa ujumbe wake. Enjoy. ... thumbnail 1 summary
Baghdad na Roma wameigeukia Singeli katika wimbo wao K waliomshirikisha Snura. Ni wimbo utakaokuvunja mbavu kwa ujumbe wake. Enjoy.


SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW:

Mkuu wa Wilaya aagiza kukamatwa mwandishi wa habari wa ITV

Mwandishi wa habari wa Kituo cha ITV mkoani Arusha, Khalfan Lihundi, anashikiliwa na polisi katika Kituo cha Polisi Usa River, wilayani A... thumbnail 1 summary
Mwandishi wa habari wa Kituo cha ITV mkoani Arusha, Khalfan Lihundi, anashikiliwa na polisi katika Kituo cha Polisi Usa River, wilayani Arumeru kwa tuhuma za kuandika habari zinazodaiwa kuwa ni za uchochezi.


Lihundi alikamatwa jana jijini hapa majira ya saa nane mchana na askari anayedaiwa kutumwa na Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Alexander Mnyeti.


Mmoja wa waandishi wa habari walioshuhudia tukio hilo, Basil Elias, alisema kuwa, walipokuwa ofisini, alifika ofisa wa polisi akidai ametumwa kumfuata Lihundi kwa ajili ya mahojiano.


Kwa mujibu wa Elias ambaye alimnukuu ofisa huyo wa polisi, Lihundi anadaiwa kuandika habari ya uchochezi kuhusu mgogoro wa maji bila kumhoji mkuu huyo wa wilaya.


“Habari hiyo inayodaiwa kuwa ni ya uchochezi, ilikuwa ni malalamiko ya wananchi juu ya tatizo la maji katika wilaya hiyo,” alisema Elias.


Akizungumzia tukio hilo, Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari, Mkoa wa Arusha (APC), Claud Gwandu, pamoja na kulaani tukio hilo, alisema hatua hiyo haikubaliki kwani haikufuata taratibu za kuadhibu mwandishi wa habari.


“Hili ni tukio la kulaani na halikubaliki kwani kama mwandishi amekosea, zinapaswa kufuatwa taratibu na siyo kukamatwa kama mhalifu.


“Kilichofanyika ni matumizi mabaya ya madaraka, hivyo viongozi wa kuteuliwa hasa wakuu wa wilaya, wawe na utaratibu wa kufuata taratibu kwani mwandishi akikosea, kuna taratibu za kufuata, tunachotaka apewe dhamana,”alisema Gwandu.


Naye Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo, alisema amesikia kuna mwandishi amekamatwa kwa kosa la uchochezi.


“Mkuu wa wilaya ametumia mamlaka yake ya sheria inayomruhusu kumweka ndani mtu hadi saa 48. Kwa hiyo, siwezi kuingilia kati suala hilo,” alisema Kamanda Mkumbo.


SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW:

Godbless Lema augua ghafla gerezani......ashindwa kufika mahakamani Kusikiliza Kesi Zinazomkabili

Kesi iliyokuwa isikilizwe 21 Disemba 2016 inayomkabili Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema pamoja na mkewe, Neema Lema wakituhumiwa kum... thumbnail 1 summary
Kesi iliyokuwa isikilizwe 21 Disemba 2016 inayomkabili Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema pamoja na mkewe, Neema Lema wakituhumiwa kumtukana Mkuu wa

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW:

HIZI NDIZO SABABU 10 ZA WANAWAKE KUTOKUOLEWA NA KUISHIIA KUSAGANA TU..

Pamoja na kuwa kuna wanawake husita kuolewa, lakini jambo hili si kubwa sana kwa wanawake kama ilivyo kwa wanaume. Kwa kiasi kikubwa kat... thumbnail 1 summary


Pamoja na kuwa kuna wanawake husita kuolewa, lakini jambo hili si kubwa sana kwa wanawake kama ilivyo kwa wanaume. Kwa kiasi kikubwa katika suala la

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW:

DIAMOND Alamba Mamilioni ya CAF, Kutumbuiza Uzinduzi wa AFCON 2017

Shirikisho la soka barani africa CAF limemchagua diamond platnumz na kumlipa mamilioni kutumbuiza kwenye shereh thumbnail 1 summary
Shirikisho la soka barani africa CAF limemchagua diamond platnumz na kumlipa mamilioni kutumbuiza kwenye shereh

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW:

Trey Songz sio role model wangu – Jux

Jux anataka watu waelewe kitu hiki ‘once and for all’, Trey Songz sio role model wake. Amedai kuwa kitendo cha kujichora tatto... thumbnail 1 summary




Jux anataka watu waelewe kitu hiki ‘once and for all’, Trey Songz sio role model wake.


Amedai kuwa kitendo cha kujichora tattoo kifuani inayofanana na msanii huyo wa Marekani, hakimaanishi kuwa ni mtu anayemuangalia kwa jicho la ‘role model.’

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW:

Izzo Bizness na Abela (The Amazing) wafunguka iwapo ni wapenzi

Izzo Bizness na Abela ni wapenzi? Hilo ni swali ambalo watu wengi wamekuwa wakijiuliza kila walisikiapo kundi la The Amazing. thumbnail 1 summary


Izzo Bizness na Abela ni wapenzi? Hilo ni swali ambalo watu wengi wamekuwa wakijiuliza kila walisikiapo kundi la The Amazing.

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW:

Mwandishi wa ITV Halfan Lihundi aachiwa kwa dhamana

Mwandishi wa habari wa ITV/Radio One Arusha Halfan Lihundi aliyekua ameshikiliwa na jeshi la polisi wilaya ya Arumeru na kuwekwa mahabus... thumbnail 1 summary
Mwandishi wa habari wa ITV/Radio One Arusha Halfan Lihundi aliyekua ameshikiliwa na jeshi la polisi wilaya ya Arumeru na kuwekwa mahabusu kwa zaidi ya masaa ishirini na manne

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW:

Wabunge wa Kenya wadaiwa kuchapana makonde Bungeni

Wabunge wa upinzani nchini Kenya wametoka bungeni kwa hasira katika mji mkuu wa Nairobi, wakisema kuwa baadhi yao walinyanyaswa bunge... thumbnail 1 summary


Wabunge wa upinzani nchini Kenya wametoka bungeni kwa hasira katika mji mkuu wa Nairobi, wakisema kuwa baadhi yao walinyanyaswa bungeni mapema asubuhi.

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW:

Donald Trump ampa shavu Peter Navarro kwenye serikali yake

R ais mteule wa Marekani, Donald Trump ameendelea na uteuzi wake kwa kuchagua baadhi ya viongozi ambao watamsaidia kuunda serikali ... thumbnail 1 summary
R

ais mteule wa Marekani, Donald Trump ameendelea na uteuzi wake kwa kuchagua baadhi ya viongozi ambao watamsaidia kuunda serikali yake wakati atakapo kabidhiwa majukumu ya kuiongoza nchi hiyo hapo mwakani.

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW:

Video: Gigy Money amtambulisha rasmi mpenzi wake, ni mtangazaji wa redio

Video Vixen Gigy Money amemtambulisha rasmi mpenzi wake na kueleza jinsi anavyompenda nakumthamini . Mtangazaji huyo wa Choice ... thumbnail 1 summary

Video Vixen Gigy Money amemtambulisha rasmi mpenzi wake na kueleza jinsi anavyompenda nakumthamini.


Mtangazaji huyo wa Choice FM ambaye pia muimbaji na hivi karibuni ameachia video mpya ya wimbo Supu akiwa na Matonya, alitembelea ofisi za Bongo5 akiwa pamoja na mpenzi wake huyo aitwae Mo J.

Akiongea na Bongo5 wiki hii Gigy Money alidai anampenda sana Mo J kwa kuwa ni mwanaume ambaye ana mpango wa kubadilia maisha yake na kumfanya awe mfanyabishara mkubwa.

“Mimi nampenda wanaume smart, handsome kama Mo J,” alisema Gigy Money. “Mo J ndo kama mume wangu, my boyfriend, na mimi nampenda kushinda kitu chochote,”

Kwa upande wa Mo J, alifunguka na kuzungumzia jinsi alivyokutana Gigy Money na kuanzisha mahusiano.

“Mimi Gigy najuana naye kama miaka 4 nyuma na kwa mara ya kwanza naonana na Gigy Gigy nilikuwa natembea na rafiki yake na kipindi hicho kuna media fulani nilikuwa nafanya kazi maeneo ya Posta. So nilikuwa nikitoka kazini namchuka mshkaji wangu tunaenda maeneo fulani. Sasa kuna siku tukawa tumepita Samaki Samaki, ndo nikaonana naye pale kwa mara ya kwanza kwa sababu alikuwa na demu ambaye nilikuwa namtokea halafu yeye ni rafiki yake,” alisema Mo J

“Baada ya kumsalimia nikavutiwa naye kwa sababu alikuwa mcheshi tofauti hata na rafiki yake ambaye alikuwa kama ananizungusha zungusha hivi, ikabidi nimtumie huyu (Gigy) nikamuuliza upo naye yule, hebu niitie, sasa Gigy ndo akawa mtu ambaye anatuonganisha. Mpaka mara ya mwisho Gigy Money ndo kama alimpush yule demu akanipa namba yake. Kwa hiyo baada ya kunipatia namba ya yule demu nikawa nawasiliana naye na pia ma nawasiliana na Gigy,” aliongeza

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW:

French Montana achukizwa na ubaguzi wa shirika la ndege la Delta

Rapper wa Marekani mwenye asili ya nchini Morocco, French Montana amesikitishwa na kitendo cha ubaguzi kilichofanywa na shirika la ndege ... thumbnail 1 summary
Rapper wa Marekani mwenye asili ya nchini Morocco, French Montana amesikitishwa na kitendo cha ubaguzi kilichofanywa na shirika la ndege la Delta Airline kwa kumshusha abiria wake kwenye ndege hiyo kwa sababu ya kuongea Kiarabu.

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW:

Wanaomshauri Darassa akatae show zile wanazoziita za ‘vichororoni’ wanataka kumwigiza choo cha kike?

Darassa ni hadithi ya mafanikio ambayo kila mdau wa muziki ataikumbuka kwa mwaka 2016. Na hadithi yake ina funzo kubwa katika namna ambay... thumbnail 1 summary
Darassa ni hadithi ya mafanikio ambayo kila mdau wa muziki ataikumbuka kwa mwaka 2016. Na hadithi yake ina funzo kubwa katika namna ambayo hit song hupatikana. Pengine nilichojifunza zaidi ni kuwa hakuna formula ya jinsi ya kupata hit.

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW: