August 31, 2014

KAMA ULIMISS STORY YA KUSIKITISHA YA KIFO CHA KIKATILI CHA MWANAFUNZI WA ZAMANI WA UDOM BETTY NDENJEMBI IKO HAPA

  Ninaandika makala hii nikitambua bayana kuwa itamuudhi kila mtu anayeingia mtandaoni kwa minajili ya kuwanyanyasa watu wengine. Lakini ... thumbnail 1 summary

 

Ninaandika makala hii nikitambua bayana kuwa itamuudhi kila mtu anayeingia mtandaoni kwa minajili ya kuwanyanyasa watu wengine. Lakini siku zote ninaamini katika busara hii: kuuchukia ukweli hakuufanyi kuwa uongo. Ukweli ni ukweli na uongo ni uongo. Ukweli hauwezi kuwa uongo, na kadhalika uongo hauwezi kuwa ukweli. Kamwe asilani.

Wakati tunaomboleza kifo cha ndugu yetu Betty Ndejembi hatuwezi kukwepa ukweli kwamba siku chache kabla ya kifo chake binti huyo alinynyaswa mno kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter. Japo hadi muda huu hatuwezi kuhusisha moja kwa moja uhusiano kati ya unyanyasaji huo na kifo cha binti huyo, ukweli tu kwamba mtu akinyanyaswa masaa kadhaa kabla ya kifo chake, waweza kujenga picha flani.



Naomba ieleweke kuwa simlaumu mtu kwa sababu sina mamlaka ya kufanya hivyo bali dhima ya makala hii ni rambirambi zangu na kuzungumzia tatizo la unyanyasaji mtandaoni, sambamba na suala zima la unafiki kila kinapojiri kifo hususan cha mtu maarufu.

Tuna tatizo kubwa huko mitandaoni. Tumefika hatua ya kuwapa umaarufu watu wenye matusi ya nguoni, wazushi, wambeya, wanafiki, wanaharamu na kila aina ya binaadamu wanaostahili laana lakini twaishia kuwatukuza. Kwa Twitter, matusi imekuwa ni njia ya mkato ya kupata umaarufu. Kuna wenzetu wengi tu wenye 'umaarufu' huko Twitter, na ukidadisi chanzo cha 'umaarufu' huo, utaambiwa 'ah huyu ana matusi si mchezo!'

Kuna watu wazima na akili zao wanatumia muda mwingi kwenye mitandao ya kijamii aidha kunyanyasa wenzao kama si kusherehesha unyanyasaji huo. Marehemu aliitwa majina kadhaa ya kumdhihaki kabla ya kukutana na mauti. Kuna waliomwita Di Maria na wanajifahamu. Japo sijui chanzo cha 'ugomvi na aliogombana nao' (na ndio maana sikujihusisha nao kwani haukunihusu), kuna wanafiki wengi tu waliokuwa katika nafasi nzuri ya kuzima moto huo hasa kwa vile baadhi yao walikuwa wakizifahamu pande zote mbili za 'ugomvi' husika.

La kukera zaidi ambalo ni wazi litajichomoza wakati wa maombolezo haya ni unafiki: baadhi ya watu walewale waliodiriki kumwandama marehemu wakati wa uhai wake watageuka kuwa wenye uchungu mkubwa baada ya kifo chake. Hii inanikumbusha suala ambalo nimeshawahi kulizungumzia mara kadhaa, katika hali ya utani japo wenye uweli, kwamba 'wakati mwafaka kabisa wa kutafuta vipaji vya uigizaji ni kwenye misiba: watu walewale waliokuwa wakikuchukia kwa nguvu zote watageuka wenye uchungu mkubwa kwa kifo chako.

Ukiangalia baadhi ya tweets za mwisho za marehemu ni wazi kuwa binti huyo alikuwa anahitaji msaada kutoka kwa wanaomjali



Hata pasi uelewa wa taaluma ya saikolojia, tweets za aina hii zinaashiria tatizo, na laiti 'wenye upendo wa dhati' wangeingilia kati muda huo, huenda muda huu Betty asingekuwa marehemu.
 


Na hizo tweets mbili ambazo ni miongoni mwa za mwisho kabisa za marehemu ni ushuhuda tosha wa jinsi alivyokuwa akisumbuliwa na wanyanyasaji dhidi yake mtandaoni. Ndio pengine kilichomuua ni maradhi ya kawaida ya kibinadamu lakini kila mwenye ubinadamu hatoshindwa kuhusisha unyanyasaji huu na hali mbaya ya afya aliyokuwa nayo hadi anafariki.


Kuna watakaolaumu kuwa ninatumia kifo cha binti huyo kwa 'maslahi binafsi.' Hapana, sina maslahi yoyote binafsi hasa ikizingatiwa kuwa sikuwa nikifahamiana na marehemu. Hakuna anani-follow na mie sikuwa nam-follow. Labda maslahi pekee niliyonayo ni upinzani wangu mkali dhidi ya unyanyasaji wa mtandaoni. Vyovyote ilivyo, marehemu alikuwa bullied kabla hajafariki na atakayetaka kukataa ukweli huo na akatae lakini utabaki kuwa ukweli usioweza kugeuka uongo. Na kwa hakika, kila aliyeshiriki kumnyanyasa binti huyo atakuwa anasutwa na nafsi yake, hata kama atatafuta hifadhi kwenye 'huu sio wakati wa kulaumiana' au 'we failed you Betty.'


Mara nyingi nimekuwa nikiwalaumu watu wanaodai 'Instagram imekuwa mbaya' au Twitter imeharibika siku hizi' ambapo mara zote nimewakumbusha wahusika kuwa katika hii mitandao ya kijamii, ni muhimu kuwa makini katika nani wa kum-follow. Maana yangu ni kwamba ukim-follow mtu mwenye matusi, utashuhudia matusi katika anachoandika. Ukim-follow mtu wa busara, utashuhudia busara.


Hata hivyo, katika siku za hivi karibuni kumeibuka kundi kubwa tu la watu wenye busara na elimu zao lakini wepesi wa kuvutiwa na vitu vya 'kipuuzi' - umbeya, matusi, majungu, na upuuzi mwingine, na hawasiti kushea na wanaowa-follow. Ni hivi, mtu akitweet tusi, kisha ukali-retweet, utambue kuwa unalikuza (amplify) tusi hilo. Na kimsingi, kwa kiasi kikubwa, tuna-RT vitu tunavyoviunga mkono. Uki-RT tusi maana yake unaliunga mkono. Na ni wazi mwenye kujiheshimu, na kuheshimu 'watu wa maana' wanaom-follow hawezi ku-RT upuuzi.


Tatizo kubwa sasa ni kwamba waweza kuamua kuwa-follow watu unaodhani wana busara au akili za kutosha lakini ukaishia kusoma vitu vya ajabu ajabu kwenye timeline yako kutokana na haya 'mahaba' ya ku-RT vitu vya kipuuzi.


Binafsi, nadhani chanzo kikubwa cha mitandao ya kijamii kuwa 'sehemu za kukera, kuogopesha, kunyanyasana, nk' ni ile hali ya baadhi ya wenzetu kutokuwa na vitu muhimu vya kufanya katika maisha yao. Ni wazi kwamba ukiwa busy na maisha yako hutokuwa na muda wa kubughudhi wenzako.


Kingine kinachopelekea social media kuwa 'dunia uwanja wa fujo' ni ugonjwa mkubwa unawasumbua baadhi ya wenzetu: kusaka sifa wasizostahili. Wanasema,. ashakum si matusi, 'lugha ya mpumbavu ni matusi,' na ndo maana baadhi ya wenzetu wasio na cha maana cha kuongea katika hadhara hukimbili matusi, unyanyasaji, maneno macha


Nitamke bayana kuwa siandiki makala hii nikitegemea kuungwa mkono na wahusika wa unyanyasaji mtandaoni. Na kwa hakika kuna uwezekano mkubwa wa makala hii kuzua 'kampeni ya chuki' dhidi yangu kutokana na makala hii. Tatizo kubwa la wenzetu hawa ni kutotaka kuambiwa kuwa 'Hapana, hili ni kosa. Na kosa ni kosa, haliwezi kuwa sahihi.' Lakini pamoja na uwezekano wa 'kuwashiwa moto' kutokana na makala hii, wito wangu kwa kila mwenye busara na akili ni kuliangalia tukio hili la kusikitisha kama 'wake up call.' Tujifunze, tujisahihishe. Tuache kusherehesha vitu vya kipuuzi mtandaoni.


Ifike mahala, ukishindwa kumkemea mtu mwenye tabia mbaya mtandaoni basi chukua option rahisi ya kum-unfollow au ikibidi kum-block. Na ifike mahala kuwafahamisha watu wanaoendekeza utoto, majungu, umbeya, unyanyasaji na upuuzi mwingine kuwa kama hawana kitu cha maana cha kufany katika maisha yao basi isiwe sababu ya kuwasumbua wenzao wenye majukumu katika maisha yao.


Tukemee maovu badala ya kutarajia yataondoka yenyewe tu. Tuomboleze kifo cha Betty kwa kusema 'NO' kwa cyberbullies (wanyanyasaji wa mtandaoni). Tufike sehemu tuache kuwasujudia wahuni wanaodhani matusi ni sehemu ya wimbo wa taifa. Tuwakwepe waendekeza majungu, wanyanyasaji, wataka sifa za kipuuzi, na watu wasiofaa katik maisha yetu.


Wakati 'tunatafuta haki kwa marehemu Betty kutokana na unyama aliofanyiwa,' suala ambalo ni la kisheria, kilicho ndani ya uwezo wetu ni kukemea unyanyasaji mtandaoni (cyber bullying). Wakati hadi muda huu hatuwajui waliomfanyia marehemu unyama huo, takriban sote twawajua vema wanyanyasaji wa mtandaoni. Tuanze na hawa, kwani leo wamefanya kwa kwa marehemu Betty kesho itakuwa kwako.


Mwisho kabisa, ni muhimu kwetu sote kutambua kuwa tulitoka kwa udongo na tutarudi kwa udongo. Kifo ni hatma ya kila mmoja wetu.Betty ametutoka lakini nasi twaelekea huko. Visa, chuki, kunyanyasana, na vitu vingine visivyopendeza japo ni kama sehemu ya maisha yetu havipaswi kupewa nafasi katika maisha yetu haya ambayo hakuna mmoja wetu mwenye japo 'lue' ya lini yatafikia kikomo. TUPENDANE na TUHESHIMIANE.


Kwako marehemu Betty, hakuna tunaloweza kusema au kufanya sasa kurejesha uhai wako. Na hakuna neno sahihi la kuonyesha jinsi gani kifo chako kimewagusa wengi. Kubwa tunaloweza kufanya ni kukuombea kwa Mwenyezi Mungu akupatie pumziko la milele na mwanga wa milele akuangazie upumzike kwa amani. Amina.

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW:

MAPENZI: BUSU SI UGOMVI...MAMBO YA KUIGA YATATUMALIZA JAMANI...!!

Hawa  jamaa  nadhani  wanahitaji  "kupigwa  pindi"  la  matumzi  ya  midomo  yao  kuhusu  "mabusu"  ambayo  ni  mila  t... thumbnail 1 summary


Hawa  jamaa  nadhani  wanahitaji  "kupigwa  pindi"  la  matumzi  ya  midomo  yao  kuhusu  "mabusu"  ambayo  ni  mila  tulizoridhi  toka  kwa  wenzetu(wazungu)...

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW:

MSONGO WA MAWAZO KIPINDI CHA UJAUZITO HUSABABISHA ULEMAVU KWA MTOTO...!! SOMA HAPA

Watafiti wa magonjwa wanadai kuwa msongo mkali wa mawazo wakati wa ujauzito unaweza kusababisha hitilafu katika uumbaji wa mtoto na hatim... thumbnail 1 summary


Watafiti wa magonjwa wanadai kuwa msongo mkali wa mawazo wakati wa ujauzito unaweza kusababisha hitilafu katika uumbaji wa mtoto na hatimaye mtoto kuzaliwa akiwa mlemavu.

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW:

HAYA NDO YALIYOJIRI KATIKA KUMTAFUTA SUPERNYOTA SERENGETI FIESTA MOSHI

Siamerary Tarimno 'Ice baby'  ambaye aliibuka kidedea katika kinyang'anyiro cha kumtafuta  Super Nyota Diva's wa Serenget... thumbnail 1 summary

Siamerary Tarimno 'Ice baby'  ambaye aliibuka kidedea katika kinyang'anyiro cha kumtafuta  Super Nyota Diva's wa Serengeti fiesta, akiimba katika shindano hilo lililofanyika kwenye Ukumbi wa Aventure Mjini

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW:

MH. MIZENGO PINDA: NI WAKATI WA JAPAN KUHAMIA AFRIKA

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Japan, Hirotaka Ishihara baada ya kukutana naye Ofisini kwak... thumbnail 1 summary

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Japan, Hirotaka Ishihara baada ya kukutana naye Ofisini kwake jijini Dar es salaam August 30, 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW:

Epl: Matokeo ya Man United vs Burnley haya hapa

Siku kadhaa baada ya kuvunja rekodi ya uhamisho kwa kulipa £60m kwa Real Madrid na kumsajili Angel Di Maria – leo hii Manchester Unit... thumbnail 1 summary

IMG_6875.JPG


Siku kadhaa baada ya kuvunja rekodi ya uhamisho kwa kulipa £60m kwa Real Madrid na kumsajili Angel Di Maria – leo hii Manchester United ilijitupa uwanjani kucheza na timu ya Burnley.

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW:

Na hii ni nyingine tena! Wasanii walioandamana nusu uchi Nairobi Kenya

Siku hizi ishu ya kuvua nguo kuonyesha msisitizo au kulipigia kelele jambo flani imekua kawaida, yani wengi wameitumia hii njia kufikisha... thumbnail 1 summary
34Siku hizi ishu ya kuvua nguo kuonyesha msisitizo au kulipigia kelele jambo flani imekua kawaida, yani wengi wameitumia hii njia kufikisha malalamiko yao na

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW:

Baada ya kuondoka kwa Torres – huyu ndio mshambuliaji mpya aliyesajiliwa na Chelsea

Usiku wa jana mshambuliaji wa kimataifa wa Spain Fernando Torres alikamilisha usajili wake wa mkopo wa miaka miwili kutoka Chelsea kw... thumbnail 1 summary

IMG_6889.JPG


Usiku wa jana mshambuliaji wa kimataifa wa Spain Fernando Torres alikamilisha usajili wake wa mkopo wa miaka miwili kutoka Chelsea kwenda AC Milan.

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW:

Inasikitisha: Mama amefariki baada tu ya kujifungua hawa Mapacha watatu.

‘Ni kweli tumepokea Watoto watatu ambao ni wachanga wakiwa na kilo 1.7 na 1.8 kutokea Misungwi, mama yao alifariki muda mfupi tu baada ya... thumbnail 1 summary
1‘Ni kweli tumepokea Watoto watatu ambao ni wachanga wakiwa na kilo 1.7 na 1.8 kutokea Misungwi, mama yao alifariki muda mfupi tu baada ya kujifungua hukohuko Misungwi na chanzo ni maamuzi yake ya kukataa kupewa matibabu

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW:

EPL: Matokeo ya Chelsea vs Everton yapo hapa

Mechi ya mwisho ya Premier League leo hii ilikuwa kati ya vijana wa Jose Mourinho Chelsea dhidi ya vijana wa Roberto Martinez Everton. thumbnail 1 summary

IMG_6886.JPG


Mechi ya mwisho ya Premier League leo hii ilikuwa kati ya vijana wa Jose Mourinho Chelsea dhidi ya vijana wa Roberto Martinez Everton.

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW:

Hii nayo kali! Ikulu ya Kenya imeongea kuhusu gari lake lililoibiwa.

Ni moja kati ya zile stori za nadra sana kuzisikia yani, kwa uoga au ulinzi mkali ambao huwa unawekwa kwenye vitu vya serikali tena sehem... thumbnail 1 summary
Screen Shot 2014-08-30 at 1.45.28 PMNi moja kati ya zile stori za nadra sana kuzisikia yani, kwa uoga au ulinzi mkali ambao huwa unawekwa kwenye vitu vya serikali tena sehemu kama Ikulu ni nadra sana kusikia kuna jamaa wamejihami na kuiba.

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW:

Epl: matokeo ya mechi zote na Kilichoikuta Man City mbele ya Stoke City hiki hapa

Mabingwa watetezi wa Ligi kuu ya England Manchester City leo wamekula mweleka katika mbio za kupigania ubingwa wao kwenye mechi dhidi... thumbnail 1 summary

IMG_6882.PNG


Mabingwa watetezi wa Ligi kuu ya England Manchester City leo wamekula mweleka katika mbio za kupigania ubingwa wao kwenye mechi dhidi ya Stoke City.

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW:

August 30, 2014

TAJIRI AFIA GESTI ARUSHA KISA NA MKASA WOTE SOMA HAPA

Tajiri mmoja aitwaye Metili amekutwa amefariki akiwa gesti ya thumbnail 1 summary
Tajiri mmoja aitwaye Metili amekutwa amefariki akiwa gesti ya

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW:

Jikumbishe amri 10 za soka enzi zetu za utoto. Lazima ucheke! SHARE na marafiki zako

Pamoja na sheria 17 za soka za FIFA kuwepo, enzi za utoto kulikuweko na sheria za soka ambazo ndizo zilizokuwa zinatambuliwa:- thumbnail 1 summary
Pamoja na sheria 17 za soka za FIFA kuwepo, enzi za utoto kulikuweko na sheria za soka ambazo ndizo zilizokuwa zinatambuliwa:-

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW:

Hii ndiyo siku Vanessa alipofunguka, kuhusu mahusiano yake yakimapenzi.

Msanii wa kike ambaye anazidi ku-make headlines hasa kwa historia yake ya kila nyimbo pale anapoi-release lazima ifanye vizuri, maarufu ... thumbnail 1 summary
Msanii wa kike ambaye anazidi ku-make headlines hasa kwa historia yake ya kila nyimbo pale anapoi-release lazima ifanye vizuri, maarufu kama Vanessa Mdee

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW:

RAIS KIKWETE AZINDUA UJENZI WA DARAJA LA GULWE MPWAPWA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete wakwanza kushoto  akiwa na Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. J... thumbnail 1 summary
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete wakwanza kushoto  akiwa na Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli, Mbunge wa Mpwapwa Mheshimiwa Gregory Teu pamoja

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW:

DAKTARI BINGWA WA MAGONJWA YA SARATANI YA MATITI KUTOKA INDIA ATOA SEMINA YA UGONJWA HUO JIJINI DAR

Daktari bingwa wa ugonjwa wa saratani ya matiti kutoka nchini India, Profesa Anthony Pais, akitoa mafunzo kuhusu ugonjwa huo kwa madaktari ... thumbnail 1 summary
Daktari bingwa wa ugonjwa wa saratani ya matiti kutoka nchini India, Profesa Anthony Pais, akitoa mafunzo kuhusu ugonjwa huo kwa madaktari wa kitanzania na wadau mbaliombakli wa sekta ya afya. Semina hiyo ilifanyika

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW:

DIVA AZIDI KUMBOMOA ZITO KABWE TAZAMA.SMS ZINGINE HAPA

Kuwa uyaone mengi sio maghorofa bali ni vituko vya binaadam katika hii dunia just imagine Zitto anavyoabika sasa hivi daaah, hivi kwel... thumbnail 1 summary
Kuwa uyaone mengi sio maghorofa bali ni vituko
vya binaadam katika hii dunia just imagine Zitto
anavyoabika sasa hivi daaah, hivi kweli kuna

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW:

VANESSA CHETTLE NA MIRFAT MUSA WA TUJUANE WABAMBWA ZAIDI WAKINYONYANA!!!!!

Vanessa Chettle  ni moja kati ya  wadada wala bata maarufu zaidi nchini Kenya....wakati Marfat Musa alikuwa maarufu baada ya kushiriki ... thumbnail 1 summary


Vanessa Chettle  ni moja kati ya  wadada wala bata maarufu zaidi nchini Kenya....wakati Marfat Musa alikuwa maarufu baada ya kushiriki kwenye kipindi

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW:

Mbowe: Mimi ni Kisiki cha CHADEMA

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe jana alikabidhiwa fomu na makada wa chama hicho na kumtaka aw... thumbnail 1 summary

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe jana alikabidhiwa fomu na makada wa chama hicho na kumtaka awanie tena kiti hicho, ombi ambalo alilikubali na kufungua milango kwa wanachama wengine ‘kupimana naye kifua’. 

“Nafasi bado ipo, anayetaka kupima kifua na mimi ajitokeze. Tena nawaomba viongozi wangu msizuie fomu kwa anayetaka,” alisema Mbowe ambaye ameongoza chama hicho kwa vipindi viwili vya miaka mitano mitano.

Makada wa chama hicho kutoka maeneo mbalimbali nchini wakiongozwa na kada maarufu, Athuman Mzigo (Mapigo Saba) kutoka Kigoma, walikutana na Mbowe na kuwasilisha maombi yao ya kumtaka awanie tena nafasi hiyo.

“Kutokana na sifa za mwenyekiti wetu, tumechangishana Sh200 kila mmoja hadi zikafika Sh50,000,” alisema Mapigo Saba huku akishangiliwa na makada wenzake alioambatana nao na kuongeza:

“Tumemwomba mwenyekiti agombee nafasi hiyo kwa kuzingatia sifa; kwanza anaijua vizuri idadi ya Watanzania na matatizo yao, pili anaungwa mkono na watu wengi na amekisaidia chama kukua. Tulikuwa na madiwani 40 leo wamefika 500, wabunge watano leo 48. Halafu hana ubaguzi ndiyo maana ameunganisha vyama vya upinzani na kuunda Ukawa (Umoja wa Katiba ya Wananchi).”

Huku akichomekea maneno ya lugha ya Kiha, Mapigo Saba alisema kuwa maombi ya kumtaka Mbowe agombee pia yametolewa katika mikoa ya Rukwa, Manyara, Iringa, Njombe, Jimbo la Same Magharibi, Zanzibar, Mwanza na Kilimanjaro.


Hotuba ya Mapigo Saba ilifuatiwa na salamu kutoka kwa wazee wa wilaya za Kinondoni, Ilala na Temeke, Baraza la Wanawake (Bawacha) na Baraza la Vijana (Bavicha).

Akitoa salamu za Bavicha, mwenyekiti wa baraza hilo Njombe, Emmanuel Masonga alisema Mbowe ni sawa na Joshua aliyemalizia kuwaongoza wana wa Israel kuingia nchi ya Kanaani:

“Sisi Wakristo tunajua kuwa Mussa alianzisha safari ya Waisrael kwenda Kanaani, ila hakuwafikisha. Kina Mtei (Edwin), Kimesera (Victor), Bob Makani na wengineo walianzisha safari ya kwenda Ikulu, ila hawakutufikisha. Mbowe ni sawa na Joshua atakayetufikisha Ikulu,” alisema Masonga.

Mwenyekiti wa Bawacha Taifa, Susan Lymo alimsifu Mbowe akisema ameongeza hamasa ya wanawake kushiriki siasa katika chama hicho.

“Mwaka 2000, kulikuwa na mwanamke mmoja katika viti maalumu, mwaka 2005 waliongezeka na kufikia sita na mwaka 2010 wamefikia 26. Mwenyekiti pia ameufanya mwaka huu kuwa wa wanawake kitaifa na ameongeza hamasa ya wanawake kushiriki siasa,” alisema Lymo.

Mbali na viongozi wa chama, alikuwapo pia Sheikh Rajab Katimba kutoka Jumuiya na Taasisi za Kiislamu ambaye alimsifu Mbowe na kuomba agombee tena nafasi hiyo.

Mbowe akubali
Baada ya Mratibu wa Vuguvugu la Mabadiliko (M4C), Nickson Tugara kummwagia sifa Mbowe, Mapigo Saba alimkabidhi fomu, huku makada wakiimba, ‘Jembe, jembe, jembe…”

Mbowe aliishukuru Kamati Kuu ya chama hicho kwa kupanga uchaguzi Septemba 14, mwaka huu ambayo ni siku yake ya kuzaliwa huku akiahidi kujenga chama imara.

“Mtaiona Chadema mpya ifikapo Septemba 14. Hiki chama hakitakufa na hatutamvumilia mtu yeyote wa kabila lolote atakayekivuruga,” alisema.

Mbowe alisema hajawahi kuomba kugombea uenyekiti wa chama hicho tangu aliponza mwaka 2000…

 “Napata wakati mgumu ninapofikia wakati huu. Chadema ina watu mbalimbali wenye taaluma na uzoefu, kwa nini mimi? Makundi haya yaliyojitokeza kunichukulia fomu yanaweza kutafsiriwa na wapenda majungu kuwa nimepanga mimi.

“Leo ni mara ya tatu naombwa kugombea uenyekiti, sijawahi kuomba. Mwaka 2004, Mzee Makani aliniomba nikamkatalia, lakini akaunda kikundi cha wazee walionichukulia fomu.

“Mwaka 2005, chama hakikuwa na mgombea urais, awali alijitokeza Profesa Mwesiga Baregu lakini akajitoa, nikaambiwa nibebe mzigo. Mwaka 2009 nikaombwa tena kugombea.”

Alisema amedhamiria kujenga chama kimtandao na kimfumo ili kuondokana na mfumo wa kienyeji… “Huko nyuma wakati wa uchaguzi watu walipeana tu nyadhifa kiundugu tukadhani chama kimeongezeka. Lakini wakati huu uchaguzi umefanyika kwa miezi tisa.

“Tulisema hatuwezi kufanya uchaguzi wa Taifa bila kupata viongozi wa mkoa, wilaya, kata, kijiji na mtaa, kitongoji na shina.

Tumefanya uchaguzi, watu wamepima na kuona mambo magumu, mara unasikia wanakimbia wakisema wameacha uenyekiti, uache wakati chama kinakua?”

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW:

HALIMA MDEE AMWAGA MACHOZI MBELE YA UMATI WA WATU KISA NA MKASA SOMA HAPA

Vigogo wa Baraza la Wanawake la Chadema (Bawacha), watachuana katika kinyang’anyiro cha kuwania uenyekiti wa baraza hilo baada ya j... thumbnail 1 summary

mdee


Vigogo wa Baraza la Wanawake la Chadema (Bawacha), watachuana katika kinyang’anyiro cha kuwania uenyekiti wa baraza hilo baada ya jana baadhi ya wanawake kujitokeza kumchukulia fomu Mbunge wa Kawe, Halima Mdee. 

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW:

ALIEKUWA DEMU WA DAVIDO, NISH KARDS AMEINGIA CLUB AKIWA MTUPU!!..CHEKI PICHAZ

Nish Kards ni  mwanadada kutoka GHANA ambae alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na msanii Davido kutoka Nigeria...maarufu sana kwenye m... thumbnail 1 summary

Nish Kards ni  mwanadada kutoka GHANA ambae alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na msanii Davido kutoka Nigeria...maarufu sana kwenye mtandao wa

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW:

Alichojibu Ronaldo kuhusu Di Maria kujiunga na Man Utd na kupewa jezi namba 7

Siku moja baada ya Angel Di Maria kutambulishwa rasmi kama mchezaji wa klabu ya Manchester United ya England huku akikabidhiwa jezi yenye... thumbnail 1 summary
Screen Shot 2014-08-29 at 10.19.11 PMSiku moja baada ya Angel Di Maria kutambulishwa rasmi kama mchezaji wa klabu ya Manchester United ya England huku akikabidhiwa jezi yenye historia kubwa ndani ya klabu hiyo (namba 7),

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW:

Baada ya ile kolabo na Rick Ross, sasa PSquare wameiachia hii video waliyoifanya na ft. T.I

Waliifanya na Rick Ross na wakachukua headlines za kutosha baada ya Akon kuwaunganisha ambapo baada ya hapo zilitoka stori nyingi za chi... thumbnail 1 summary
Screen Shot 2014-08-29 at 9.09.53 PMWaliifanya na Rick Ross na wakachukua headlines za kutosha baada ya Akon kuwaunganisha ambapo baada ya hapo zilitoka stori nyingi za chinichini kwamba wakali hawa wa Nigeria

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW:

Shinji Kagawa njiani kuondoka Man United – hii ndio klabu anayoenda

Wakati wa utambulisho rasmi wa Angel Di Maria jana, kocha qa man United Louis Van Gaal alithibitishqa kwamba kuna kundi la wachezaji lit... thumbnail 1 summary
1409307188735_wps_2_File_photo_of_Manchester_
Wakati wa utambulisho rasmi wa Angel Di Maria jana, kocha qa man United Louis Van Gaal alithibitishqa kwamba kuna kundi la wachezaji litaondoka mpaka kufikia mwishoni mwa wiki hii.

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW:

Hatimaye Torres amua kuondoka Chelsea – hii ndio tiku aliyoichagua

Fernando Torres amemaliza kipindi kigumu kabisa cha miaka mitatu na nusu kwenye maisha yake ndani ya klabu ya Chelsea baada ya kukuba... thumbnail 1 summary

IMG_6865.JPG


Fernando Torres amemaliza kipindi kigumu kabisa cha miaka mitatu na nusu kwenye maisha yake ndani ya klabu ya Chelsea baada ya kukubali kuondoka katika timu hiyo.

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW:

JIDE, DOGODOGO GUMZO MJINI! DOGO ANASWA NA MKOKO WAKE

OHOOO!  Siku chache baada ya ndoa ya Legendary wa Bongo Fleva, Judith Wambura Mbibo ‘Jide’ na mtangazaji mahiri nchini, Gardner Gabriel H... thumbnail 1 summary
OHOOO! Siku chache baada ya ndoa ya Legendary wa Bongo Fleva, Judith Wambura Mbibo ‘Jide’ na mtangazaji mahiri nchini, Gardner Gabriel Habash ‘G Habash’ kudaiwa kuvunjika, gumzo limeibuka kufuatia kunaswa kwa picha za

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW:

MKEATELEKEZWA NA MSANII KIKONGWE CHIDUMULE CHANZO SOMA HAPA

Mke wa mkongwe wa Nyimbo za Injili Bongo, Rev. Cosmas Chidumule aliyejitambulisha kwa jina la Cesilia Maiko na wanaye, wanadai kutelekezwa ... thumbnail 1 summary
Mke wa mkongwe wa Nyimbo za Injili Bongo, Rev. Cosmas Chidumule aliyejitambulisha kwa jina la Cesilia Maiko na wanaye, wanadai kutelekezwa na staa huyo huku mama huyo akiandamwa na maradhi ya kisukari.

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW:

DIVA, AUNT KIMENUKA CHANZO UJAUZITO!

JAMBO  limezua jambo! Staa wa sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel Grayson amemvaa prizenta wa Kipindi cha Ala za Roho cha Redio Clouds FM, Lo... thumbnail 1 summary
JAMBO limezua jambo! Staa wa sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel Grayson amemvaa prizenta wa Kipindi cha Ala za Roho cha Redio Clouds FM, Lovennes Malinzi ‘Diva’ kwa madai kwamba amemtangaza mitandaoni kuwa

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW:

WASTARA JUMA AZICHAPA NA MUMEWE MAHAKAMANI

WIKI iliyopita katika makala haya tuliishia pale mwigizaji Wastara Juma alivyokimbizwa na mumewe wa kwanza na kuokolewa na difenda la polis... thumbnail 1 summary
WIKI iliyopita katika makala haya tuliishia pale mwigizaji Wastara Juma alivyokimbizwa na mumewe wa kwanza na kuokolewa na difenda la polisi, TUENDELEE…

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW:

ZAMARADI MKETEMA ASEMA NDOTO YAKE YA KUASILI MTOTO SABABU SOMA HAPA

Host wa Program ya Take One kupitia CloudsTV, Zamaradi Mketema ametangaza nia yake kuwa anataka kuasili mtoto ili kutimiza ndoto yake thumbnail 1 summary
Host wa Program ya Take One kupitia CloudsTV, Zamaradi Mketema ametangaza nia yake kuwa anataka kuasili mtoto ili kutimiza ndoto yake

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW:

MSAIDIZI WA MWINGIRA ALIVYOUAWA KWA RISASI

INASIKITISHA!  Mchungaji kiongozi wa Kanisa la Efatha, Nabii Josephat Mwingira, mwishoni mwa wiki alimpoteza mkalimani wake, Adson Philip C... thumbnail 1 summary
INASIKITISHA! Mchungaji kiongozi wa Kanisa la Efatha, Nabii Josephat Mwingira, mwishoni mwa wiki alimpoteza mkalimani wake, Adson Philip Cheyo aliyeuawa kwa kupigwa risasi katika viwanja vya Mlimani City jijini Dar es Salaam.

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW:

SAKATA.LA OKWI KUTIMUKIA SIMBA MANJI AJA JUU

BAADA ya jana uongozi wa timu ya Simba chini ya Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili , Zacharia Hans Pope , kutangaza kumsainisha mshambu... thumbnail 1 summary
BAADA ya jana uongozi wa timu ya Simba
chini ya Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ,
Zacharia Hans Pope , kutangaza kumsainisha
mshambuliaji , Emmanuel Okwi , raia wa

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW:

August 29, 2014

NUH MZIWANDA WA SHILOLE ALIKOPI KWA NICK CANNON NA MARIAH CAREY KUWEKA TATTOO? AMEPATA MFANO!

Mwimbaji wa Bongo Flava, Nuh Mziwanda aliwashitua wengi baada ya kujichora tattoo yenye jina la mpenzi wake ‘Shilole’, tattoo ambay... thumbnail 1 summary


Mwimbaji wa Bongo Flava, Nuh Mziwanda aliwashitua wengi baada ya kujichora tattoo yenye jina la mpenzi wake ‘Shilole’, tattoo ambayo haifutiki daima. Kitu ambacho kiliwashitua wengi.

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW:

ILE VIDEO YA NEY INAYOHUSISHWA NA FREEMASON KWA PICHA ZAKE ZA AJABU, IMETOKA. ICHEKI HAPA

Video Mpya ya Nay wa Mitego iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu kutoka na Picha za Ajabu zilizotoka wakati wa uchukuaji wa Video hiyo, Itazam... thumbnail 1 summary
Video Mpya ya Nay wa Mitego iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu kutoka na Picha za Ajabu zilizotoka wakati wa uchukuaji wa Video hiyo, Itazame hapa Chini alafu

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW:

Boss wa TBS aliyehukumiwa kwenda jela miaka mitatu.

Mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu Dar es Salaam August 28 2014 imetoa hukumu kwa aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Viwango Tanzani... thumbnail 1 summary
Screen Shot 2014-08-29 at 8.32.31 AMMahakama ya Hakimu mkazi Kisutu Dar es Salaam August 28 2014 imetoa hukumu kwa aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Viwango Tanzania (TBS) Charles Ekerege kifungo cha miaka 3 jela.

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW:

Good news!! baada ya Abu Dhabi sasa Clouds media International imeingia Jamaica

Kwanza shukrani zikufikie popote ulipo ewe mtu wa nguvu ambae siku zote umekua ukiisupport na kuwa karibu na Clouds Media. thumbnail 1 summary
Screen Shot 2014-08-29 at 9.03.39 AMKwanza shukrani zikufikie popote ulipo ewe mtu wa nguvu ambae siku zote umekua ukiisupport na kuwa karibu na Clouds Media.

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW:

CHUJI ASAKWA MCHANGANI BAADA YA KUTOROKA NA SH 60000...NJAA KALI KWELI

ALIYEKUWA kiungo wa Yanga , Athuman Idd ‘ Chuji ’ inaelezwa kuwa ameingia mitini na fedha kiasi cha shilingi 60 ,000 za timu ya Mazom... thumbnail 1 summary
ALIYEKUWA kiungo wa Yanga , Athuman Idd
‘ Chuji ’ inaelezwa kuwa ameingia mitini na
fedha kiasi cha shilingi 60 ,000 za timu ya
Mazombi FC ya Gongo la Mboto ambazo
alipewa kwa ajili ya kuichezea katika nusu
fainali ya Kombe la Ng’ ombe .

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW:

POLISI AMGONGA MTOTO, ATOKA NDUKI, ATELEKEZA GARI

POLISI  mmoja ambaye hakufahamika jina lake mara moja, aliyekuwa akiendesha gari kwa mwendo wa kasi, Jumapili iliyopita alimgonga mtoto w... thumbnail 1 summary
POLISI mmoja ambaye hakufahamika jina lake mara moja, aliyekuwa akiendesha gari kwa mwendo wa kasi, Jumapili iliyopita alimgonga mtoto wa kike, Zahara Almeda katika barabara ya Mji Mpya.

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW:

SHEMEJI WA WEMA ATANGAZA NDOA NA DADA WA DIAMOND

MAPENZI bwana!  Baada ya kuogelea kwa muda mrefu katika penzi la muigizaji Kajala Masanja, hatimaye shemeji wa aliyekuwa rafiki wa mwigiz... thumbnail 1 summary
MAPENZI bwana! Baada ya kuogelea kwa muda mrefu katika penzi la muigizaji Kajala Masanja, hatimaye shemeji wa aliyekuwa rafiki wa mwigizaji huyo, Wema Sepetu, Ahmed Hashimu ‘Petit Man’ ametangaza ndoa na dada wa Mbongo

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW:

SABBY: RUSHWA YA NGONO BONGO MUVI IMENITESA

Msanii wa filamu, Salma Omary ‘Sabby’ ameamua kufunguka kuwa ameteswa sana na rushwa ya ngono aliyokuwa akikutana nayo pindi alipokuwa thumbnail 1 summary
Msanii wa filamu, Salma Omary ‘Sabby’ ameamua kufunguka kuwa ameteswa sana na rushwa ya ngono aliyokuwa akikutana nayo pindi alipokuwa

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW: