June 14, 2014

MWANAMKE AMKUMBATIA MAHAKAMANI MTU ALIYEMUUA MWANAE

Kama kuna kitu ambacho wengi wameshindwa  kuimudu kutokana na hisia zao ni kumsamehe adui  yako tena aliyesababisha umpoteze mwanao. M... thumbnail 1 summary

Kama kuna kitu ambacho wengi wameshindwa kuimudu kutokana na hisia zao ni kumsamehe adui yako tena aliyesababisha umpoteze mwanao.

Mama mmoja mkaazi wa Florida, Marekani ameonesha moyo wa huruma alipokuwa mahakamani baada ya kumkumbatia kwa upendo Jordyn Howe mwenye miaka 16 aliyekutwa na hatia

ya kuua kwa kumpiga risasi mtoto wa mama huyo aliyekuwa na umri wa miaka 13 mwaka 2012. Maelezo yaliyotolewa mahakamani hapo na muendesha mashitaka yalidai kuwa Jordyn Howe
alikuwa na umri wa miaka 14 aliichukua bastola ya baba yake wa kambo na kwenda nayo shuleni ambapo alifika na kuanza kumfanyia utani rafiki yake aitwa Lourdes Guzman –DeJesus aliyekuwa na miaka 13. Howe alijaribu kufyatua risasi chini kwenye ardhi na Bahati nzuri hakuna kilichofanyika na risasi
haikutoka, baada ya kuona hivyo alimnyooshea bunduki rafiki yake kiutani lakini wakati huu alipofyatua risasi ilitoka kweli na kumpiga Lourdes, tukio lililopelekea kifo chake. Baada ya kusomewa mashitaka mtoto huyo alikiri
mara moja kufanya kosa na kumuua rafiki yake na kisha kuomba msahama. “Nasikitika kwa kumuondoa na naomba radhi kwa kufanya kile nilichokifanya.” Alisema. Maelezo ya mama huyo yalimuingia moyoni na ikambini aseme huku akiishiwa maneno. “Ni uzoefu unaoumiza sana.” Alizungumza huku
akiwa anatetemeka mikono. “Wazazi wawili hawatakiwi….hapana…siwezi.” Mtoto huyo alipewa kifungo cha miezi 22 gerezani. Mwanzoni mama wa mtoto aliyepigwa risasi aliitaka mahakama kumpa adhabu kali, lakini baada ya
maelezo hayo alibadili msimamo na kumkumbatia mtoto huyo kisha kuzungumza na hakimu namna nyingine ya kuyamaliza. Hakimu aliamuru mtoto huyo kutumia mwaka mmoja
katika kituo/mahakama ya watoto na kisha yeye na mama huyo watapewa nafasi ya kuzunguka Florida wakihamasisha watu kuachana na matumizi ya silaha za moto. “Nimemsamehe kwa sababu nimekuwa na amani, kwa sababu nahisi kama binti yangu sasa hivi yuko katika sehemu ya amani. Siwezi kumrudisha mwanangu, lakini angalau naweza kulitunza jina lake kuwa hai.”

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW: