June 14, 2014

DAWA ZA NYWELE ZINAZOSABABISHA UVIMBE WA KIZAZI KWA WANAWAKE

Dawa za kulainisha nywele (relaxer) zimekuwa zinapendwa na wanawake wengi wa Afrika kwa kuwa zina uwezo wa kulainisha nywele na kumfan... thumbnail 1 summary

Dawa za kulainisha nywele (relaxer)
zimekuwa zinapendwa na wanawake
wengi wa Afrika kwa kuwa zina uwezo wa
kulainisha nywele na kumfanya apendeze
na awe wa kuvutia.
Hata hivyo, wataalamu wa afya wanadai
kuwa dawa hizo zinasababisha uvimbe

kwenye kizazi kutokana na kemikali za
dawa hizo ambazo huingia mwilini kupitia
majeraha au ngozi wakati wa kupaka.
Daktari wa Manispaa ya Ilala, Laurent
Chipata alifanya utafiti na kubaini kuwa
dawa za nywele na vipodozi zina kemikali
ambazo husababisha uzalishwaji wa
vichocheo kwa kiasi kikubwa na
kusababisha uvimbe kwenye kizazi uitwao
fibroids au leimyoma.
"Kemikali hizi hupenya kwenye ngozi na
wakati mwingine hata kwa harufu tu,
husababisha kuzalishwa kwa wingi wa
vichocheo aina ya estrogen ambavyo
huchangia kuota kwa uvimbe wa fibroids,"
anasema.
Dk Chipata anasema kukua kwa uvimbe
kwenye kizazi hutokea katika kipindi
ambacho mama yupo kwenye uzazi yaani
kabla hajakoma hedhi.
Utafiti wa Dk Chipata ulifanywa nchini na
kujumuisha wanawake wa kada tofauti
tofauti wanaotumia dawa za nywele na
wale wasiotumia na ukubwa wa tatizo hili
ulibainika.
"Zipo kemikali tofauti tofauti
zinazosababisha uvinbe kwenye kizazi, zipo
za kwenye dawa za kilimo kama DDT na za
kwenye mafuta ya ngozi kama vile mercury
na hydroquionone," anasema.
Dk Chipata anasema madhara
yanayopatikana katika kemikali za vipodozi
ni makubwa siyo tu kwenye kizazi bali
nyingine husababisha saratani au kufeli
kwa figo. Anatoa mfano wa kemikali ya
zebaki (mercury).
"Dawa za nywele
zina madhara si lazima
zipenye kwenye ngozi baada ya mtu kupata
jeraha la kuungua bali zinaweza kupenya
zenyewe kwenye ngozi kutokana na
mfumo wa ngozi," anasema.
Anashauri kuwa ni vyema watu wakasoma
kipodozi kimetengenezwa kwa nini kabla
ya kukitumia na kuongeza kuwa ni salama
zaidi kubaki na ngozi au nywele halisi
badala ya kujibadilisha.
Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA)
imekataza vipodozi vyenye kemikali kama
biothionol, hexachlorophene, mercury, vinyl
chloride, zirconium na bidhaa zenye
aerosol, chloroquionone, steroids,
methylene na chloroform.
Utafiti mwingine uliofanywa mwaka 2012
na Dk Lauren Wise na wenzake nchini
Marekani na kuchapishwa kwenye jarida la
afya la nchini Marekani ulibaini kuwa
vipodozi vingi vina kemikali zenye
vichocheo vya estrogen ambavyo kwa
kawaida huchochea kasi ya kuota kwa
uvimbe kwenye kizazi cha mwanamke na
wakati mwingine kwenye mji wa mimba.
Kitaalamu uvimbe au vivimbe hivi hujulikana
kama fibroids au myoma.

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW: