June 14, 2014

FLORA MBASHA NJIA YA PANDA, WACHUNGAJI WADAI HAWAWEZI KUHUDUMIWA NA MWIMBAJI MZINZI

Mpasuko  wa  ndoa  ya  wasanii  wa  nyimbo  za  Injili, Emmanuel  Mbasha  na  mkewe  Florah  umewagawa  wachungaji  wa  makanis... thumbnail 1 summary



Mpasuko  wa  ndoa  ya  wasanii  wa  nyimbo  za  Injili, Emmanuel  Mbasha  na  mkewe  Florah  umewagawa  wachungaji  wa  makanisa  mbalimbali  nchini  baada  ya  kibao  kumgeukia  Flora  kwamba  ndiye  anadaiwa  kusuka  mpango  wa  kumwangamiza  mumewe  ili  afungwe  kwa  kosa  la  ubakaji…..
Wakizungumza  na  wanahabari  wetu  kwa  nyakati  tofauti,  wachungaji  hao  walisema  endapo  itabainika  ni  kweli  Flora  ameshiriki  kumsaliti  mumewe  kwa  kutembea  na  mmoja  wa  wachungaji  maarufu    nchini  hapatakuwa  na  haja  ya  kumwalika  kwenye  huduma  zao  kwani  hawawezi  kuhudumiwa  na  mwimbaji  mzinzi.

Mchungaji  Ambonile  Mwakipesye  na  Amani  Joseph  wa  makanisa  ya  Tanzania  Assemblies  of  God ( TAG)   walisema  kuwa  kama  kulikuwa  na  matatizo  kwenye  ndoa  yao  walipaswa  kuwaona  watumishi  wa  Mungu  na  kusuluhisha  badala  ya  kutengenezeana  mitego  na  kuingizana  majaribuni  kama  inavyodaiwa  kutokea  kwa  Mbasha….


Wakati  wachungaji  hao  wakisema  hivyo, mchungaji  Thomas  Methew  yeye  alisema  kuwa  ukweli  wa  jambo  hilo  wanaujua  wanandoa  wenyewe  kwani  mpaka  sasa  hakuna  anayelijua  tatizo  kubwa  mpaka  wakafikia  hatua  ya  kutengana

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW: