June 14, 2014

Full time ya Spain vs Holland – matokeo na wafungaji haya hapa

Michuano ya kombe la dunia imezidi kushika kasi kwa michezo miwili iliyopigwa leo. Mchezo wa kwanza leo hii ulikuwa kati ya wawakil... thumbnail 1 summary

20140614-000651-411661.jpg

Michuano ya kombe la dunia imezidi kushika kasi kwa michezo miwili iliyopigwa leo.


Mchezo wa kwanza leo hii ulikuwa kati ya wawakilishi wa Afrika Cameroon dhidi ya Mexico, na wamexico wakaondoka na ushindi wa goli moja kwa bila.

Mechi ya pili iliyomalizika hivi punde ilishuhudia mabingwa watetezi Spain wakidhalilishwa kwa
kipigo kizito kutoka kwa Uholanzi.
Spain walianza kuliona lango la Uholanzi kwa mkwaju wa penati wa Xabi Alonso, lakini Robin van Persie akaisawazishia Uholanzi kabla ya mapumziko.
Kipindi cha pili Uholanzi walirudi kwa kasi na kufanikiwa kuongeza magoli mengine manne kupitia Van Persie, Robben aliyefunga mawili
na beki Stephan de Virj akaongeza la tano. Mpira ukamalizika kwa Spain kufungwa 5-1.
Saa 7 usiku kutakuwa na mchezo wa mwisho wa leo hii kati ya Chile vs Australia.

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW: