June 15, 2014

ALIKIBA AFUNGUKA SABABU YA KUKAA KIMYA KWA MIAKA MITATU

Kwa muda mrefu wafuasi wa mwanamuziki Ally Salehe Kiba maarufu Alikiba, wamekuwa wakijiuliza sababu zilizomfanya mwimbaji huyo kukaa k... thumbnail 1 summary

Kwa muda mrefu wafuasi wa mwanamuziki
Ally Salehe Kiba maarufu Alikiba, wamekuwa
wakijiuliza sababu zilizomfanya mwimbaji
huyo kukaa kando ya muziki kwa muda
mrefu.
Alikiba ambaye aliachia wimbo wake wa
mwisho "My Everything" Novemba 2012
hajawahi kuachia tena wimbo mwingine,
licha ya kutoa kazi kadhaa alizokuwa

akishirikishwa na mdogo wake msanii
Abdu Kiba ukiwamo "Kidela".
Starehe ilikaa kitako na msanii huyu
aliyewahi kutamba na wimbo wake wa
kwanza "Sinderela" mwaka 2007,
nyumbani kwake Kunduchi Beach na
ambapo aliainisha mambo makubwa
matatu yaliyomfanya asimame kwa muda
kuachia kazi za muziki.
"Kuna mambo matatu ya msingi niliyokuwa
nayafanya kwa kipindi hiki cha miaka
mitatu. Awali ya yote niliamua kusimama ili
kumlea mwanangu, malezi ya mtoto
yalinifanya niegemee huko hadi umri wake
usogee ndipo nirudi kwenye muziki,"
anasema pasipo kufafanua vizuri iwapo ni
wa kike au wa kiume.
Anasema familia yake ni kitu chenye
uthamani mkubwa kwake ndiyo maana
alijitoa ili kuhakikisha inakaa sawa.
"Jambo la pili ambalo najivunia kulifanikisha
kwa kipindi hiki, ni kuweza kumsimamisha
sehemu nzuri mdogo wangu Abdu Kiba
katika ramani ya muziki. Hili lilikuwa suala
kubwa na nyeti kwangu kuhakikisha
anatimiza ndoto zake
nilijitahidi kumpa
nyenzo ili na yeye ajulikane kwani
nilimuona ana kipaji kikubwa," anasema.
Jambo la tatu analifafanua kuwa ilimchukua
muda kufikiria namna atakavyowaacha
wasanii wengine Tanzania, na wao
wajulikane ndani na nje ya nchi.
"Tatu niliona nitulize kichwa kidogo kwa
kufanya biashara na pia kuwaacha wasanii
wengine na wao kipaji chao kionekane na
kuwapa nafasi ya kufanya vizuri ndani na
nje ya nchi, nashukuru hilo limefanikiwa
tena kwa kiasi kikubwa, kwa kuwa kwa
kipindi hicho wameibuka wengi ambao
wameweza kufanya vizuri na kwa wale
ambao walikuwepo kitambo wamepanuka
zaidi kifikra, " anasema Alikiba.
Anasema kwa kipindi cha miaka mitatu
aliyopumzika, amejifunza mengi na pia
ameona kumekuwa na mapungufu katika
tasnia ya muziki wa kizazi kipya na
maendeleo pia.
"Mapungufu yamekuwepo, lakini kuna
mafanikio mengi pia, kuna baadhi ya
wasanii wamefanikiwa kufanya muziki
mzuri na kuutangaza kimataifa na wengine
wametengeneza kazi nzuri, lakini
kinachonitisha ladha ya muziki wetu asili
hasa ya bongofleva, imepotea tumeanza
kutengeneza muziki wenye utofauti
mkubwa sana na kipindi cha nyuma, kwa
kuiga ala ya
muziki wa Nigeria na mataifa
mengine," anasema Alikiba.
Albamu mbili, singo mpya wiki ijayo
Alikiba aliyetamba na wimbo "Dushelele"
miaka miwili iliyopita, ameweka wazi ujio
wake wiki ijayo akiwa chini ya kampuni
kubwa barani Afrika ambayo hajataka
kuiweka wazi, anasema alikuwa 'chimbo'
kwa takribani miaka miwili akiandaa kazi
mpya ambapo amefanikiwa kukamilisha
albamu mbili na punde kuachia singo mpya.

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW: