June 15, 2014

ALIKIBA AFUNGUKA BAADA YA KUKAA KIMYA KWA MIAKA MITATU, NA HII NDIYO TAREHE ATAYOTOA WIMBO WAKE MPYA..!!


Kwa muda mrefu wafuasi wa mwanamuziki Ally Salehe
Kiba maarufu Alikiba, wamekuwa wakijiuliza sababu
zilizomfanya mwimbaji huyo kukaa kando ya muziki
kwa muda mrefu. Alikiba ambaye aliachia wimbo wake wa mwisho “My Everything” Novemba 2012 hajawahi kuachia tena wimbo mwingine, licha ya kutoa kazi kadhaa alizokuwa
akishirikishwa na mdogo wake msanii Abdu Kiba
ukiwamo “Kidela”. Starehe ilikaa kitako na msanii huyu aliyewahi kutamba
na wimbo wake wa kwanza “Sinderela” mwaka 2007,
nyumbani kwake Kunduchi Beach na ambapo
aliainisha mambo makubwa matatu yaliyomfanya
asimame kwa muda kuachia kazi za muziki. “Kuna mambo matatu ya msingi niliyokuwa
nayafanya kwa kipindi hiki cha miaka mitatu. Awali
ya yote niliamua kusimama ili kumlea mwanangu,
malezi ya mtoto yalinifanya niegemee huko hadi umri
wake usogee ndipo nirudi kwenye muziki,” anasema pasipo kufafanua vizuri iwapo ni wa kike au wa kiume. Anasema familia yake ni kitu chenye uthamani mkubwa
kwake ndiyo maana alijitoa ili kuhakikisha inakaa
sawa. “Jambo la pili ambalo najivunia kulifanikisha kwa
kipindi hiki, ni kuweza kumsimamisha sehemu nzuri
mdogo wangu Abdu Kiba katika ramani ya muziki.
Hili lilikuwa suala kubwa na nyeti kwangu
kuhakikisha anatimiza ndoto zake nilijitahidi kumpa
nyenzo ili na yeye ajulikane kwani nilimuona ana kipaji kikubwa,” anasema.

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW: