June 15, 2014

COSTA RICA YAICHEZESHEA KICHAPO URUGUAY 3 - 1 ....HUKU SUAREZ AKIWA NJE NA MAJONZI

Costa Rica wakiwashukuru mashabiki baada ya ushindi wa bao 3-1 dhidi ya Uruguay. thumbnail 1 summary
Costa Rica wakiwashukuru mashabiki baada ya ushindi wa bao 3-1 dhidi ya Uruguay.

Majonzi: Luis Suarez (wa kwanza kulia) aliyekuwa benchi akiwa haamini kilichotokea.
Edinson Cavani akiifungia Uruguay bao lao pekee.
KIKOSI cha Uruguay kimelala kwa bao 3-1 dhidi ya Costa Rica katika mechi ya kundi D kwenye Fainali za Kombe la Dunia 2014 zinazoendelea nchini Brazil. Katika mechi hiyo, mshambuliaji mahiri wa Uruguay na Liverpool Luis Suarez alikuwa benchi.
Wafungaji wa Costa Rica waliopeleka maumivu Uruguay ni Joel Campbell, Oscar Duarte na Marcos Urena. Uruguay walipata bao lao kwa mkwaju wa penalti kupitia kwa Edinson Cavani.

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW: