May 20, 2016

MIRUNGI KILO 500 YAKAMATWA,JE KUGAWIWA??

Jeshi la Polisi mkoani Mara linawashikilia wakazi wawili wa Mtaa wa Nyegezi, Wilaya ya Nyamagana, Mkoa wa Mwanza kwa tuhuma za kusafiri... thumbnail 1 summary

Jeshi la Polisi mkoani Mara linawashikilia wakazi wawili wa Mtaa wa Nyegezi, Wilaya ya Nyamagana, Mkoa wa Mwanza kwa tuhuma za kusafirisha dawa za kulevya aina ya mirungi.


Kamanda wa Polisi mkoani humo, Ramadhani Ng’anzi alisema jana kuwa watuhumiwa hao walikamatwa Mei 17, saa nane mchana katika Kijiji cha Mulyaza wilayani Butiama wakiwa na kilo 500 za dawa hizo zimehifadhiwa kwenye vifurushi 15 yenye uzito wa zaidi ya nusu tani.


Alisema watuhumiwa hao walikuwa wakisafirisha dawa hizo kwa kutumia gari aina ya Toyota Carina lililokuwa likiendeshwa na mmoja wao wakitokea Sirari, Wilaya ya Tarime wakielekea Mwanza.


Hata hivyo, aliwaomba wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa jeshi hilo ili kusaidia kuwakamata watu wanaokiuka sheria na taratibu za nchi.


Baadhi ya wakazi wa mjini hapa walisema udhibiti wa dawa za kulevya ni jukumu la kila Mtanzania kwa sababu madhara yake husababisha athari katika jamii inayozunguka eneo husika.

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW:

No comments