May 20, 2016

Feza Kessy Anahisi Makampuni Yanapenda Kuwapa Endorsement Mastaa Wenye Skendo!

Feza Kessy amesema anashangaa jinsi ambavyo makampuni nchini yameshindwa kuwatumia mastaa mbalimbali kwenye kazi za ubalozi kama zilivyo ... thumbnail 1 summary
Feza Kessy amesema anashangaa jinsi ambavyo makampuni nchini yameshindwa kuwatumia mastaa mbalimbali kwenye kazi za ubalozi kama zilivyo nchi zingine Afrika. 
Akiongea kwenye kipindi cha Take One cha Clouds FM Jumanne hii, mtangazaji huyo wa Choice FM alisema makampuni mengi yanafanya kazi kwa mazoea na yanaogopa kufunguka zaidi. 

“I feel like corporate wanaogopa, kwa mfano ni brand fulani let’s say ya simu ikamtumia the biggest artist lakini unaangalia nchi zingine kama Nigeria unakuta that same company ina artists 20,” alisema Feza. 

Feza alisema alichogundua ni kuwa makampuni mengi yanapenda kuwatumia mastaa wenye skendo na wanaoandikwa sana magazetini. “Wanapenda kutumia artists ambao kidogo ni scandalous,” alisisitiza. 

Alisema kwa mfano alipokuwa Botswana aliweza kuzunguka kwenye shule nyingi kuongea na wanafunzi ambao walikuwa wakimsikiliza sana. “Lakini hapa Tanzania utakuta I am here na hawatanitumia, hawakuoni sababu labda sipo kwenye magazeti ya udaku.” 

Alitolea pia mfano jinsi ambavyo hadi sasa hakuna kampuni ambayo imemtumia Idris Sultan ipasavyo pamoja na kuwa na ushawishi mkubwa si tu Tanzania bali Afrika nzima kutokana na kuwa mshindi wa Big Brother Africa. 

Mrembo huyo pamoja na kuwa muimbaji na mtangazaji amekuwa akijihusisha na shughuli za kijamii kusaidia waathirika wa madawa ya kulevya.

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW:

No comments