May 20, 2016

Lady Jaydee Kumweka Wazi Mrithi wa Gardner Leo, Ipo Hapa

Mkongwe wa Bongo Fleva kwa zaidi ya miaka kumi na tano, Judith Wambura Mbibo ‘Lady Jaydee au Jide’, anatarajia kumuanika mrithi wa aliyek... thumbnail 1 summary
Mkongwe wa Bongo Fleva kwa zaidi ya miaka kumi na tano, Judith Wambura Mbibo ‘Lady Jaydee au Jide’, anatarajia kumuanika mrithi wa aliyekuwa mumewe, Mtangazaji wa Kituo cha Radio CloudsFM, Gardner G. Habash ndani ya saa 24, Ijumaa lina data kamili.

Kwa mujibu wa habari za kuaminika zilizothibitishwa na uongozi wa staa huyo, Jide atamtambulisha mchumba wake huyo kwa mara ya kwanza ndani ya Ukumbi wa Mlimani City leo, Dar ambapo pia atafanya shoo ya saa tatu mfululizo, inayokwenda kwa jina la Naamka Tena.

“Itakuwa ‘sapraizi’ kwa mashabiki wote wa Jide ambapo sapraizi hii itaendana na shoo ya kihistoria ya Naamka Tena atakayoipiga kwa saa tatu akiwa na bendi yake (Lady Jaydee and The Band),” alisema mmoja wa viongozi wanaomsimamia ambaye hakutaka kutajwa gazetini.

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW:

No comments