May 13, 2016

Nyota ya Wizkid yazidi kung’aa Ulaya

Staa wa muziki kutoka Nigeria, Wizkid amepata dili la kufanya show London kwenye tamasha Wireless Festival 2016 litakalofanyika mwezi Jul... thumbnail 1 summary
Staa wa muziki kutoka Nigeria, Wizkid amepata dili la kufanya show London kwenye tamasha Wireless Festival 2016 litakalofanyika mwezi Julai mwaka huu. Tamasha hilo ambalo hufanyika kila mwaka jijini London, mwaka huu litawakutanisha mastaa wengine kama Future, Big Sean, Fergie, Calvin Harris, Chase & Status na J.Cole.

Nyota ya Wizkid inaonekana kuzidi kung’aa baada ya siku chache kuonekana kwenye list ya Billboard Hot 100 Top 10 kupitia wimbo alioshirikishwa na Drake ‘One Dance’ kushika namba moja kwenye chati hizo.

Mwaka jana tamasha hilo la Wireless Festival liliwajumuisha mastaa kama, DJ David Guetta, Kendrick Lemar, Gorgon City, Drake na Nicki Minaj.

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW:

No comments