May 13, 2016

Maamuzi mapya ya Chelsea juu ya nahodha wake John Terry

Klabu ya soka ya Chelsea leo May 13 2016 imeamua kutangaza maamuzi ambayo yalikuwa hayatarajiwi na wengi, kuhusu nahodha wake na beki wak... thumbnail 1 summary
Klabu ya soka ya Chelsea leo May 13 2016 imeamua kutangaza maamuzi ambayo yalikuwa hayatarajiwi na wengi, kuhusu nahodha wake na beki wake wa kati John Terryambaye ameichezea klabu hiyo kwa zaidi ya miaka 15, klabu leo imeamua kumpa nafasi ya kuongeza mkataba wa mwaka mmoja wa kuendelea kuitumikia klabu hiyo.

John Terry mkataba wake unamalizika mwisho wa msimu huu, lakini mwezi January aliweka wazi kuwa ataondoka Chelsea kwa maana hatoongeza mkataba tena, lakini taarifa zilizotoka leo May 13 2016, ni kuwa klabu na mchezaji huyo wamekubaliana kuongeza mkataba wa mwaka mmoja.

Terry akiwa ndani ya klabu ya Chelsea toka mwaka 1998, amefanikiwa kucheza jumla ya mechi 703, mwaka 2005 John Terry alijumuisha katika kikosi bora cha dunia kilitangazwa na Shirikisho la soka duniani FIFA (FIFAPro World XI).

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW:

No comments