June 13, 2014

Wizi NMB Mwanga: Wakenya wawili wahukumiwa kunyongwa hadi kufa

Raia wawili wa Kenya, Samweli Saitoti (Saimoo) na Michael Kimani (Mike), wamehukumiwa kunyongwahadi kufa baada ya kupatikana na hatia y... thumbnail 1 summary

Raia wawili wa Kenya, Samweli Saitoti (Saimoo) na Michael Kimani
(Mike), wamehukumiwa kunyongwahadi kufa baada ya kupatikana na hatia
ya kumuua polisi wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), PC Michael
Milanzi mwaka 2007.Raia hao ambao walipambana na polisi jijini Arusha
kwa saa sita wakijihami kwa silaha za kivita yakiwamo mabomu ya

kurusha kwa mkono na bunduki aina ya Sub Machine Gun (SMG), walifanya
mauaji hayo yaliyoambatana na uporaji wa Sh239 milioni mali ya Benki
ya NMB, Julai 11, 2007.Pia, Jaji Kakusulo Sambo wa Mahakama Kuu Kanda
ya Moshi, amemhukumu Mtanzania, Calist Kanje kwenda jela miaka mitano
kwa kuwasaidia wauaji hao wasikamatwe na polisi baada ya kufanya
mauaji.Akitoa hukumu hiyo jana, Jaji Sambo alisema upande wa mashtaka
ukiongozwa na Wakili
waSerikali, Ladslaus Komanya, Stella Majaliwa na
Ignas Mwinuka, umethibitisha mashtaka hayo pasipo shaka.Jaji Sambo
alisema ushahidi wa mashahidi 18, umethibitisha kuwa raia hao wa Kenya
ndiyo walioshirikiana kwa pamoja, kumuua polisi huyo ambaye taifa bado
lilikuwa likihitaji utumishi wake."Kulikuwa na hoja ya utetezi kuwa
hawakutambuliwa kikamilifu lakini PC Naftali Ashery aliyekuwa lindo na
marehemu aliwatambua vilivyo wauaji hao tena kwa
ukaribu,"alisema.Alisema Mahakama imeridhika kuwa maungamo waliyoyatoa
mbele ya walinzi wa amani ambao ni mahakimu waliyatoa kwa hiari bila
kushurutishwa.Mahakama imeukataa utetezi wa washtakiwa hao kuwa wakati
wa mauaji hawakuwa nchini, akisema ushahidi wa vinasaba (DNA),
umethibitisha walikuwapo nyumbani kwa mshtakiwa Kanje.Jaji alisema kwa
kuwa washtakiwa hao walikwenda kwa Kanje na yeye
akawasaidia
wasikamatwe na kuwatorosha, hilo ni kosa la kusaidia wahalifu baada ya
kufanyamauaji.Jaji Sambo alisema Kanje ndiye aliyeficha gari aina ya
Toyota Land Cruiser mali ya Mahakama ya Kimataifa ya Rwanda (ICTR),
lililotumika katika ujambazi huo na kwamba ushahidi wa wafanyakazi
wawili wa mshtakiwa huyo, unathibitisha kuwa ndiye aliyetoa maelekezo
kwa dereva wake ili akalitelekeze gari hilo eneo la Uwanja wa Ndege wa
KIA.Mahakama hiyo imeamuru kiasi cha fedha, Dola 8,145 za Marekani na
Sh1,769,000 walizokutwa nazo raia hao wa Kenya, zikabidhiwe Benki ya
NMB, Mwanga zilikoibwa.Credit: Mwananchi 

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW: