June 13, 2014

JE, UNAFAHAMU NINI KUHUSU USAJILI WA NDOANA TARAKA?

AINA ZA NDOANdoa ya mke mmoja, mume mmoja au inayokusudiwa kuwa ya mke mmoja, mumemmoja, na ndoa ya wake wengi au inayokusudiwa kuwa ya ... thumbnail 1 summary

AINA ZA NDOANdoa ya mke mmoja, mume mmoja au inayokusudiwa kuwa ya mke
mmoja, mumemmoja, na ndoa ya wake wengi au inayokusudiwa kuwa ya wake
wengi.Mamlaka ya kufungisha ndoa nchini Tanzania Bara yako mikononi
mwa:Ndoa za serikali, wakuu wa wilaya na makatibu tawala wa wilaya
ndio wenyemamlaka kisheria ya kufungisha ndoaNdoa za kidini,

hufungishwa na viongozi wa dini (maaskofu, mapadri, wachungaji,
masheikh)wenye leseni hai za kufungisha ndoaNdoa za kimila,
hufungishwa mbele ya afisa mwandikishaji (afisa tarafa) husika wa
sehemu ile ndoa inapofungia.NdoaYEYOTEiwe ya serikali,kidini,kimila
kabla ya kufungwa lazima itangazwe kwa siku 21.Matangazo haya yatolewe
kwa namna ambayo itawezesha umma kujua taarifa za ndoa inayotarajiwa
kufungwa,ili kama kuna pingamizi liweze kuwasilishwa.Baada ya siku 21
kupita bila pingamizi,msajili mkuu wa ndoa.Kusajili ndoa,ni jukumu la
mfungishaji ndoa kuisajili ndoa aliyoifungisha na kuwapatia vyeti
wanandoa.Ndoa isajiliwe kwa kujaza fomu RGMF 7 na baada ya kuijaza
wanandoa watatia saini wakifuatiwa na wasimamizi wao na mfungishaji
ndoa atawapatia wana ndoa nakala ya kwanza ya shahada ya ndoa kila
mmoja.Nakala ya pili iwasilishwe kwa msajili mkuu wa ndoa na talaka
kila mwisho wa mwezi huo ziwezwe kuandikishwa kwenye daftari la ndoa
la msajili mkuu wa ndoa na
talaka.Umuhimu wa kusajili talaka ni kama
ifuatavyo;kutoa utambulisho kwa wanandoa kuwa ni mke na mume,cheti cha
ndoa kinampa mwanandoa haki ya urithi endapo mwenzi wake
atafariki,cheti cha ndoa ndio uthibitisho wa ndoa kisheria,cheti cha
ndoa kinamwezesha mwanandoa kupata nafuu ya kodi,cheti chandoa kinampa
mtoto aliyezaliwa ndani ya ndoa haki ya kurithi pasipo wosia.Usajili
wa talakaTalaka ni ruhusa au amri ya mahakama ya kisheria ambayo mume
au mke hupewa wakati anapomwacha mwenzi wake.Chombo chenye mamlaka ya
kutoa talaka ni mahakama tu.Baada ya ndoa kuvunjwa mahakama inatakiwa
kuwasilisha nakala ya uamuzi (decree) ya kuvunja ndoa au kubadilishwa
kwa ndoa kwa msajili mkuu wa ndoa na talaka kwa ajili ya kusajiliwa
kwenye daftarila talaka na kutoa hati ya talaka,au ubatilisho wa
kuvunjika kwa ndoa.Kwa waumini wa dini za kiislamu.TALAKA zitolewazo
kwa msingi wa dini ya kiislamu huwa hazivunji ndoa iliyofungwa chini
ya sheria ya ndoa.Talaka za jinsi hii kisheria zinaangaliwa kama ni
nia ya kutoa talaka.Talaka itawasilishwa mahakamani ambayo itatamka
kuvunjika kwa ndoa. Mahakama itatoa uamuzi ambao mhusika atatumia
kusajili maamuzi ya kuvunjika kwa ndoa yake kwa msajili mkuu wa ndoa
na talaka.Hatua za kufuata wakati wa kuomba talakaMwombaji
wa talaka
lazima afuate taratibu zifuatazo;Kwanza, mwenye nia ya kuomba talaka
atapeleka malalamiko ya matatizo yake kwenye baraza la usuluhishi wa
ndoa kwenye ofisi ya kamishina wa ustawi wa jamii au baraza la kata,
kanisani ama BAKWATA. Pili,baraza la usuluhishi la ndoalitasikiliza
malalamiko na kama likishindwakusuluhisha,hati maalum itaandikiwa
kwenda mahakamani ikieleza mgogoro huona kutoa maoni yake kuhusu suala
husika.Tatu,walalamikaji/mlalamikaji atapeleka hati hiyo mahakamani
kufungua shauri la kuomba ndoa ivunjwe kisheria na staili zake
kutamkwa.Faida za kusajili talaka ni;kumwezesha mtalakiwa kupata haki
ya kuoa au kuolewa tena,kuwezesha umma kujua kuwa ndoa
imevunjika,kulinda mali ya mtalaka endapo atafariki na mtalakiwa kudai
urithi,kupata takwimu za ndoa zinazovunjika na wapi zinatokea.Kwa
maelezo zaidi kuhusu masuala ya usajili wa ndoa,talaka,na leseni za
ndoa wasiliana kwa anuani ifuatayo;AFISA MTENDAJI MKUU/KABITHI WASII
MKUUWAKALA WA USAJILI,UFILISI NA UTHAMINI{RITA}MTAA WA
KIPALAPALA,KIWANJA NA.516,UPANGAS.L.P 9183,DAR-ES-SALAAM.SIMU
NAMBA:255222153069

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW: