December 16, 2016

Trailer: Jay Z akamilisha filamu yake ya kijana aliyejiua akiwa na miaka 22

Rapper Jay Z amekamilisha stori ya filamu yake fupi ya kijana aliyejipiga risasi itakayoanza kuruka kwenye runinga kuanzia mwakani. thumbnail 1 summary



Rapper Jay Z amekamilisha stori ya filamu yake fupi ya kijana aliyejipiga risasi itakayoanza kuruka kwenye runinga kuanzia mwakani.


Makala hiyo iliyopewa jina la ‘TIME: The Kalief Browder Story’ imetokana na historia ya kweli ya kijana mwenye mika 22 aliyejipiga risasi na kujiua mwaka jana, Kalief Browder.

Wakati Kijana huyo akiwa na miaka 16 alituhumiwa kwa kosa la kuiba begi na kupelekwa jela ya Rikers Island ya mjini New York huku kesi yake ikikaa kwa kipindi cha miaka miwili bila ya kusikilizwa, wakati huo huo aliwekwa kwenye chumba cha giza kwa muda mrefu sana na baadaye akaachiwa.

Makala hiyo imeandaliwa na Jay Z pamoja na Harvey Weinstein na inatarajiwa kuanza kuruka kupitia Spike kuanzia Machi 1 mwakani. Tazama trailer la filamu hiyo hapa chini.

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW:

No comments