December 16, 2016

Bow Wow aingia kwenye bifu zito na Dj Funkmaster

Rapper Bow Wow ameingia kwenye bifu zito na Dj maarufu wa New York, Funkmaster Flex. Bifu hilo limeibuka baada ya Dj huyo kumdiss Bow W... thumbnail 1 summary
Rapper Bow Wow ameingia kwenye bifu zito na Dj maarufu wa New York, Funkmaster Flex.
Bifu hilo limeibuka baada ya Dj huyo kumdiss Bow Wow kwenye mtandao wake wa Twitter kwa kumtaja kuwa ni msanii ambaye hajielewi na hafanyi vizuri kutokana na albamu zake hazinunuliwi na mashabiki.

“FYI- Bowwow is Fucking finished out here! FACTS! His records is trash! Basura!,” ameandika Dj Funk kwenye moja ya post zake kwenye mtandao huo.

Baada ya muda Bow Wow alijibu mapigo kwa kurushiana maneno na Dj huyo na kuitaa redio anmayofanyia kazi Dj huyo kumfukuza na kuajiri watu wengine. Mwisho rapper huyo alimblock Dj huyo ambaye anadaiwa kupenda kutupiana maneno na wasanii, mmoja kati ya watu wengine aliowahi kuingia kwenye bifu nao ni Drake.

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW:

No comments