December 16, 2016

Chuchu Hansy: Muda ukifika watu watajua kama nina mimba au sina

Muigizaji wa kike filamu Bongo, Chuchu Hansy amefunguka sababu ya kuficha ujauzito wake. Chuchu ameiambia EATV kuwa ameamua kufanya hivyo... thumbnail 1 summary
Muigizaji wa kike filamu Bongo, Chuchu Hansy amefunguka sababu ya kuficha ujauzito wake.
Chuchu ameiambia EATV kuwa ameamua kufanya hivyo kwa kuwa hivyo huwa ni vitu vya mtu binafsi ila muda ukifika kila kitu kitakuwa wazi.

“Unajua vitu kama hivyo ni too personal na nisingependa kuviongelea especially kwenye media. Lakini muda muafaka ukifika kila mmoja atajua nini ni nini, ila kwa sasa acha ikae hivyo watu waendelee kuhisi,” amesema muigizaji huyo.

Chuchu alifanikiwa kushinda tuzo ya muigizaji bora wa kike kwenye tuzo za Eatv Awards 2016 zilizotolewa Jumamosi iliyopita.

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW:

No comments