April 21, 2016

Chris Brown Ataka Kujiua!

Chris Brown Mwanamuziki Chris Brown amesema kuwa alitaka kujiua baada ya kumshambulia aliyekuwa mpenziwe Rihanna kabla ya tuzo za Gram... thumbnail 1 summary
chris-brown-2015-tumblr-wallpaper-4
Chris Brown
Mwanamuziki Chris Brown amesema kuwa alitaka kujiua baada ya kumshambulia aliyekuwa mpenziwe Rihanna kabla ya tuzo za Grammy mwaka 2009.
Katika kipande kifupi cha makala yake ya ‘Welcome to My Life’, mwanamuziki huyo wa R & B amesema kuwa uhusiano wao ulikuwa kama ndoto lakini akajihisi kama hayawani.

”Nilikuwa katika kilele cha dunia,nyimbo zangu zikiongoza,nikapendwa na wengi nchini Marekani kabla ya kuanguka hadi kuwa adui wa uma”, alisema Breezy.

chris-brown-rihanna-2008-600x407
Rihanna na Chris Brown
Brown alihukumiwa kifungo cha miaka mitano jela kufuata shambulio hilo. Kifungo hicho kilisitishwa mwaka jana baada ya jaji moja kusema kuwa nyota huyo amekamilisha mahitaji yake yote na kufunga kesi hiyo rasmi.
Makala hiyo inayowaonyesha Jennifer Lopez,Usher, Mike Tyson, Jamie Fox na Rita Ora, Chris Brown anasema kuwa ”Nilihisi kama nyota, lakini nilijiharibia”.
”Nilikuwa nikilala. Sikuweza kula,nilijihisi maarufu”,alikiri.

Tazama Documentaty Trailer ya Welcome to My Life

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW:

No comments