April 21, 2016

Cheki Video: Hali ya CHID BENZ Yazidi Kuimarika

BAADA ya kumaliza mwezi mmoja akipata matibabu, afya ya rapa Chid Benz imeendelea kuimarika kila kukicha kufuatia tiba anayoendelea kuipa... thumbnail 1 summary
BAADA ya kumaliza mwezi mmoja akipata matibabu, afya ya rapa Chid Benz imeendelea kuimarika kila kukicha kufuatia tiba anayoendelea kuipata katika Kituo cha Rehab Bagamoyo. Kalapina amepost short clip video ikionesha hali ya rapa huyo akiwa anaendela vyema. 


Alichokisema Chid Benz

“Sina mengi ya kuongea, niko poa niko okay, niko sawa yani niko fresh na msaada ninaupata vizuri, na ninaendelea vizuri.

Meneja wa Diamond, Babutale akishirikiana Kalapina walimpeleka Chidi Benz kwenye Kituo cha Life and Hope Rehabilitation Organization kilichopo Bagamoyo kwa ajili kumsaidiwa kuacha matumizi ya madawa ya kulevya.

Hatua hiyo ilikuja baada ya rapa huyo kuomba msaada baada ya kuona ameshindwa kukabiliana na matatizo ya kiafya ambayo yamekuwa yakimkabili.

Watanzania tuendelee kumuombea Chid Benz ili afya yake iendelee kuimarika na hatimaye apone kabisa na mwi8sho wa siku tujiunge naye katika ujenzi wa Taifa letu. 

A video posted by KalApina harakati (@kalapina) on Apr 19, 2016 at 9:53am PDT

Siku alipopelekwa Kituo cha Rehab, Bagamoyo kwa ajili ya tiba.

A video posted by KalApina harakati (@kalapina) on Mar 22, 2016 at 9:50am PDT

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW:

No comments