August 28, 2014

ROONEY NAHODHA MPYA ENGLAND

KOCHA wa England, Roy Hodgson amemteua mshambuliaji wa Manchester United, Wayne Rooney kuwa nahodha mpya wa timu hiyo ya taifa. thumbnail 1 summary
KOCHA wa England, Roy Hodgson amemteua mshambuliaji wa Manchester United, Wayne Rooney kuwa nahodha mpya wa timu hiyo ya taifa.

Rooney mwenye miaka 28 amechukua mikoba iliyoachwa na kiungo wa Liverpool, Steven Gerrard aliyestaafu.


Rooney aliwahi kuvaa kitambaa cha unahodha akiiongoza England kwenye mechi ya kufuzu kucheza Kombe la Dunia dhidi ya San Marino, Oktoba 2012.
Staa huyo amewapiku wachezaji wenzake kipa Joe Hart na beki Gary Cahill ambao nao walikuwa wakitajwa kuchukua uongozi huo.

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW: