August 26, 2014

MASKINI,MKE WAKAMANDA BARLOW NUSRA AUAWE KWA MAWE

UONEVU!  Ikiwa imepita takribani miaka miwili tangu aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, ACP Liberates Barlow (53) (picha ndogo) ... thumbnail 1 summary

UONEVU! Ikiwa imepita takribani miaka miwili tangu aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, ACP Liberates Barlow (53) (picha ndogo) afariki dunia usiku wa Oktoba 13, 2012 kwa kupigwa risasi na watu waliodhaniwa ni
majambazi,  mke wa marehemu, Stella Barlow naye yamemkuta mazito kwani chupuchupu auawe.
Mke wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, ACP Liberates Barlow (53), Stella Barlow (wa pili kulia) akiomboleza katika mazishi ya mume wake.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, Jumatano ya Agosti 13, mwaka huu mjane huyo anayeishi jijini Mwanza alikwenda Moshi Vijijini mkoani Kilimanjaro kwenye kaburi alilozikwa mumewe kwa ajili ya kulijenga lakini cha ajabu ndugu wa marehemu walimfukuza kwa mapanga na marungu na kumtaka aondoke eneo hilo mara moja.
Chanzo kilisema kuwa, ndugu hao walimfukuza huku wakidai kwamba awalipe pesa kwa ajili ya eneo hilo la kaburi alilozikwa mumewe kwa vile marehemu hakuzikwa kwenye eneo lake, jambo ambalo ilidaiwa kuitia aibu familia hiyo.
Makamanda wa Polisi wakitoa heshima za mwisho wakati wa mazishi ya ACP Liberates Barlow.

Uwazi lilimsaka msemaji wa ukoo bila mafanikio lakini mtu mmoja aliyedai si msemaji akiomba kuhifadhiwa jina lake alisema kilichotokea ni mwanamke huyo kutaka kuonesha anajua sheria wakati ukoo ulitaka kila kitu kiende kwa uzuri na utaratibu.
“Sisi hatukuwa na nia mbaya, kila mtu anajua mila za Kilimanjaro, sasa tulitaka kuweka mambo sawa, yeye akawa anataka kutuonesha anajua sheria,” alisema mtu huyo.
Juzi, Uwazi lilimsaka kwa njia ya simu mjane wa marehemu huyo ambapo alipopatikana alikuwa na haya ya kusema:
Marehemu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, ACP Liberates Barlow (53) enzi za uhai wake
“Ni kweli tukio hilo lilitokea nilikwednda kwenye kaburi la mume wangu kwa ajili ya kufanya maombi lakini nilizuiliwa na ndugu wakisema kwamba hawataki kuniona kwa sababu mume wangu alizikwa pale kimakosa.
“Hata hivyo, walinitimua huku wengine wakinitishia kwa mapanga lakini sijachukua hatua yoyote ila  nimemwachia Mungu.”

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW: