June 01, 2016

Young Killer adai Khaligraph yupo real, ni baada ya kumtaja kama rapper wa Bongo anayependa kumshirikisha

Baada ya Khaligraph rapper kutoka Kenya kutoa ya moyoni kuwa Young Killer ndio rapper a nayevutiwa kufanya naye kazi kwa muda toka alivyom... thumbnail 1 summary
Baada ya Khaligraph rapper kutoka Kenya kutoa ya moyoni kuwa Young Killer ndio rapper anayevutiwa kufanya naye kazi kwa muda toka alivyomfahamu, hitmaker huyo wa Dear Gambe amedai amefarijika sana baada ya kusikia hivyo.


“Nimefurahishwa sana baada ya kusikia taarifa hizi na ninaweza kusema tu Khaligraph ameniwahi kwani naye ni miongoni mwa wasanii ambao nina ndoto ya kufanya nao kazi,” Young Killer alisema kwenye Story 3 za Planet Bongo ya EA Radio.

“Khaligraph yupo real sababu kuna watu wengine wanakuwa wanapenda kazi zako lakini kusema ndio inakuwa issue lakini Khaligraph ameamua awe real na nitafanya naye ngoma ili nizidi kujiongezea mashabiki zaidi,” aliongeza rapper huyo.

Khaligraph ni rapper anayefanya vizuri kutoka Kenya na anaingia katika list ya wasanii waliofanya cover nzuri ya wimbo Ojuelegba wa Wizkid.

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW:

No comments