June 01, 2016

Nyumba ya Michael Jackson yatangazwa kuuzwa

Hatimaye nyumba ya aliyekuwa staa wa muziki wa Pop duniani, Michael Jackson imetangaza kuuzwa. Nyumba hiyo iliyopo eneo la Nevada huko La... thumbnail 1 summary
Hatimaye nyumba ya aliyekuwa staa wa muziki wa Pop duniani, Michael Jackson imetangaza kuuzwa.
Nyumba hiyo iliyopo eneo la Nevada huko Las Vegas imetangazwa kuuzwa na familia ya marehemu kwa dau la dola milioni 9.5. Aliyekuwa meneja wa staa huyo [Kristen Routh] amethibitisha kuuzwa kwa nyumba hiyo yenye eneo la mraba 24,276 huku ikiwa na vyumba saba vya kulala, mabafu 12 na eneo jingine kubwa.

Aidha imeelezwa kuwa fedha zitakazo patikana kwenye mauzo ya nyumba hiyo zitawezesha kusaidia watoto wa marehemu aliowaacha ambao ni Prince Michael Jackson II, Paris-Michael Katherine Jackson na Michael Joseph Jackson Jr.

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW:

No comments