June 01, 2016

Fid Q alia na wasanii wa Hip Hop wanaoshindwa kuuendesha muziki wao kibiashara

Msanii wa muziki wa Hip Hop, Fareed Kubanda ‘Fid Q’ amesema chanzo cha kuanguka kwa muziki wa Hip Hop kunasababishwa na wasanii wenyewe. ... thumbnail 1 summary
Msanii wa muziki wa Hip Hop, Fareed Kubanda ‘Fid Q’ amesema chanzo cha kuanguka kwa muziki wa Hip Hop kunasababishwa na wasanii wenyewe.
Akiongea katika kipindi cha Enewz cha East Africa Television Jumatatu hii, Fid Q amesema wasanii wengi wa Hip Hop wanafanya video za kawaida kabisa ambazo zinashindwa kwendana na soko la muziki huku wakikaza zaidi kwenye nyimbo zao.

“Shida ya muziki wa Hip Hop bongo ililetwa na bajeti kuwa ndogo kwenye video zetu, unakuta msanii ana bonge la dude lakini video yupo maskani anacheza kamari na masela. Kwa hiyo tukashindwa kudeal na biashara inayoendelea sasa hivi, maana biashara saizi imetoka kwenye show bizz imekwenda kwenye ‘eye candy’ watu wanahitaji wanahitaji kutazama vitu ambavyo vinawavutia kwenye macho yao. Ndiyo maana unakuta watu kama mimi saizi tunakwea pipa tunakwenda Africa Kusini kushoot video tukiwa na warembo wazuri,” alisema Fid Q

Aliongeza, “Kitu kingine kitendo cha kushindwa kuwekeza kwenye video zetu ni sawa na kujishusha wenyewe, leo hata ukiandaa tamasha nakwambia watu wengi wanakuja kwenye tamasha hilo wanakuja kusikiliza na kuona wazee wa Hip hop waje kufanya yao na si hawa wasanii wa bongo fleva hivyo kama watawekeza kwenye video itasaidia Bongo hip hop kukuwa zaidi ndani na nje ya nchi,” aliongeza Fid Q

Rappa huyo kwa sasa anafanya poa na video yake ya wimbo, ‘Walk It Off’ iliyoandaliwa nchini Afrika Kusini.

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW:

No comments