June 02, 2016

Breaking News: Wabunge Wote wa Upinzani Watoka Nje Kupinga Naibu Spika Kuendesha Vikao vya Bunge.

Wabunge wote wa vyama vya upinzani leo tena wametoka nje kupinga Naibu Spika wa Bunge Dk. Tulia Ackson kuendesha vikao vya Bunge na kumwa... thumbnail 1 summary
Wabunge wote wa vyama vya upinzani leo tena wametoka nje kupinga Naibu Spika wa Bunge Dk. Tulia Ackson kuendesha vikao vya Bunge na kumwachia Bunge yeye na wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Taarifa kutoka Bungeni zinaeleza kuwa, wabunge wote wa upinzani wametoka nje kususia kikao cha Bunge ikiwa ni kutekeleza azimio lao la kutokuwa na imani na Dk Tulia.

Baada tu ya kusomwa dua ya kufungua Bunge, wabunge hao wametoka nje majira ya saa 3:00 asubuhi na kumwacha Dk. Tulia akiwa na wabunge wa CCM pekee.

Kambi upinzani ilianza utaratibu huo juzi kwa kutoka ndani ya ukumbi wa Bunge baada ya Dk. Ackson kuingia ukumbini.

Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, juzi alisema wataendelea kutoshiriki vikao vinavyoongozwa na Naibu Spika hadi pale "haki itakapopatikana."

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW:

No comments