May 18, 2016

Wewe ni Bingwa wa kupiga Selfie? mtazame huyu alivyoweka rekodi yake

Kijana Hugo Cornellier raia wa Canada ameingia kwenye headlines baada ya kugundulika kuwa amekuwa na desturi ya kujipiga picha (selfie) kwa... thumbnail 1 summary

Kijana Hugo Cornellier raia wa Canada ameingia kwenye headlines baada ya kugundulika kuwa amekuwa na desturi ya kujipiga picha (selfie) kwa muda wa miaka nane na nusu mfululizo tangu akiwa na miaka 12 mpaka alipofikisha miaka 20, yeye amedai kuwa alihitaji kuona mabadiliko katika maisha yake ya kila siku swala ambalo sio wengi wanalifanya.

Hugo Cornellier alitengeneza video ambayo alizichanganya picha zote alizozipiga kila siku na katika matukio maalum katika maisha yake kama vile siku ya kwanza kuwasili shule, msichana wa kwanza kuwa na mahusiano naye pamoja na siku ya kwanza kazini alipoajiriwa.

Tazama video aliyotengeneza Hugo kwa kutumia picha zote alizopiga kwa miaka nane mfululizo.

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW:

No comments