May 19, 2016

Sevilla watwaa kombe la Europa kwa kuifunga Liverpool

Timu ya soka ya nchini Hispania, Sevilla FC imefanikiwa kutwaa taji la Europa League kwa mara ya tatu mfululizo baada ya kuifunga Liverpool... thumbnail 1 summary
Timu ya soka ya nchini Hispania, Sevilla FC imefanikiwa kutwaa taji la Europa League kwa mara ya tatu mfululizo baada ya kuifunga Liverpool kwenye hatua ya fainali.

Liverpool ndiyo walikuwa wa kwanza kupata goli dakika ya 35 kupitia kwa mshambuliaji wake Sturridge, lakini kipindi cha pili kilipoanza Sevilla walionekana kuja juu na kufanikiwa kusawazisha goli hilo dakika 46 kupitia kwa Gameiro.

Aidha Liverpool walishindwa kuizuia kasi ya Wahispania hao baada ya kuruhusu magoli mengine mawili kwenye dakika ya 64 na 70 kupitia kwa Coke. Mpaka mpira unamalizika matokeo yalibaki 3-1.

Hata hivyo kocha wa Liverpool, Jorge Klopp amesema kuwa amekuwa hana bahati na michezo ya fainali kwa hii ilikuwa ni fainali yake ya sita na kupoteza.

Mashindano ya Ulaya msimu huu yatatawaliwa na vilabu vya Hispania, huku ikisubiriwa mchezo wa fainali wa Ligi ya Mabingwa Ulaya (UEFA) utakaochezwa Mei 28 mwaka huu kati ya Atletico Madrid dhidi ya Real Madrid.

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW:

No comments