December 17, 2016

Serikali yataka machinga wawekewe utaratibu mzuri wa kufanya biashara

Serikali imewataka wakuu wa mikoa, wilaya na mamlaka ya serikali za mitaa na miji kuweka utaratibu na mfumo utakaowasaidia wafanya bi... thumbnail 1 summary


Serikali imewataka wakuu wa mikoa, wilaya na mamlaka ya serikali za mitaa na miji kuweka utaratibu na mfumo utakaowasaidia wafanya biashara wadogo wadogo (wamachinga) kufanya biashara
zao kwa kuzingatia utaratibu mzuri ili kuwawezesha kujipatia kipato cha kuendesha maisha yao na familia zao.


Wito huo umetolewa mjini Dodoma na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), George Simbachawene na kusisitiza kuwa wamachinga wana haki ya kufanya kazi zao kwa utaratibu mzuri na mamlaka za serikali zinapaswa zitambuwe mchango wao katika uchumi.

“Lazima wajipange kutekeleza maagizo ya mheshimiwa rais kwa ufasaha,weledi na umakini mkubwa ili kuwasaidia ndugu zetu wamachinga kufanya biashara zao kujipatia kipato cha kuendesha maisha yao na familia zao na waagia wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya na mamlaka za serikali za mitaa kuhakikisha zinatekeleza agizo la mheshimiwa rais na sio kususia na kuwaacha wamachinga wafanye biashara zao kiholela,” alisema Simbachawene.

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW:

No comments