May 16, 2016

Ni kweli Harmonize amemrithi Diamond kwa Jacqueline Wolper?

Wanasema sharing is caring. Ndiyo maana Harmonize haoni hatari kuweka kambi kwenye koloni la zamani la bosi wake, Diamond. Inaonekana s... thumbnail 1 summary
Wanasema sharing is caring. Ndiyo maana Harmonize haoni hatari kuweka kambi kwenye koloni la zamani la bosi wake, Diamond.
Inaonekana si tetesi tena kwasababu CEO wa WCB mwenyewe ametoa baraka zake kwa wawili hao, Harmonize na Jacqueline Wolper ambao yeye anawaita ‘love birds.’ Diamond na Wolper waliwahi kuwa na uhusiano miaka kadhaa iliyopita.



Muimbaji huyo wa ‘Make Me Sing’ amepost video inayomuonesha Harmonize akiwa kwenye gari na mpenzi wake huyo mpya huku akimuimbia hit ya bosi wake, Number One.


“A throw Back of two love Birdsbirdrevolving_hearts…. Mjini kutamu jamani… hebu nitagie Wakereketwa hapa, waje kuzirai….?” ameandika Diamond kwenye video hiyo.

Naye dada yake, Esma hakusita kulipigia chapuo penzi hilo jipya kwa kuiweka video hiyo na kuandika: Karibu ktk familia yetu @wolperstylish mawifi tunagubu but utuzoee ila nawee usije kuwa na roho mbaya mjengoni mchaga wewe harmo wetu tumetoka nae mbaliii tangu tunalala stendi winkmaskmaskmask utuzalie twaribu maana kwetu ni T T tuuu mawifi wazamani am soleeee kaka kashapenda tunafanyaje msiniblokuuu tuu tupendane japo kinafki bana.”

Hata hivyo si wote wanaoshare furaha hiyo huku wengi wakidai kuwa Harmonize anahitaji kuwa na msichana wa size yake.

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW:

No comments