February 23, 2016

Hii huenda ikawa dalili nyinigine ya Mourinho kujiunga na Man United, kafanya maandlizi haya

Headlines za kocha wa zamani wa vilabu vya Real Madrid na Chelsea ya UingerezaJose Mourinho February 23 ameingia kwenye headlines baada y... thumbnail 1 summary
Headlines za kocha wa zamani wa vilabu vya Real Madrid na Chelsea ya UingerezaJose Mourinho February 23 ameingia kwenye headlines baada ya kuonesha viashiria vingine vya kuwa anakaribia kuhamia jiji la Manchester ambalo ndio makao makuu ya klabu ya Man United yalipo.

Jose Mourinho tayari anatajwa kutafuta na kupata nyumba ya kuishi katika jiji laManchester na baadhi ya magazeti mengine yameandika kuwa tayari kapata nyumba na yupo katika mchakato wa kununua vitu vya ndani. Klabu ya Man United ambayo ipo nafasi ya 5 katika msimamo wa Ligi Kuu Uingereza kwa kuwa na point 41 .

Gazeti la Ureno Correio da Manha ni moja kati ya magazeti yalioandika stori hii.

Hivyo uongozi hauridhishwi na uwezo wa kocha wao wa sasa Louis van Gaal, hivyo wanatajwa kuwa watamfuta kazi mwisho wa msimu na kumpa nafasi Jose Mourinho. Kama Mourinho atajiunga na Man United, hiyo itakuwa ni klabu yake ya pili yaUingereza kuifundisha na ya sita kwa ujumla toka amekuwa kocha.

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW: