July 16, 2014

CHEKA KISHAROBARO: KAMA WEWE MUONGO HATA UKISEMA UKWELI BADO UTAONEKANA MWONGO TUUU .... USTAKE NCHEKE HAPA

Jamaa mmoja mwenye mke alikuwa na mahusiano na sekretari wake. Siku moja walipotoka kazini akajisahau na kuondoka na sekretari wake nyumb... thumbnail 1 summary
Jamaa mmoja mwenye mke alikuwa na mahusiano na sekretari wake. Siku moja walipotoka kazini akajisahau na kuondoka na sekretari wake nyumbani kwa sekretari.

Baada ya kazi zilizowapeleka kule kuisha akapitiwa na usingizi na kushtuka saa mbili usiku. Yule jamaa akamwambia yule sekretari achukue viatu (vya mwanaume) avisugue sugue katika nyasi hadi vionekane vina rangi ya kijani kijani. Kisha yule jamaa akachukua shati lake na kurudi nyumbani. Alipofika nyumbani na kumkuta mkewe mazungumzo yalikuwa kama yafuatayo;

Mke: Ulikuwa wapi tangu ulipotoka kazini saa nane mchana?
Mume: Mke wangu siwezi kukudanganya hata kidogo, nilikuwa nyumbani kwa sekretari wangu mimi na yeye tunakula raha na baada ya hapo nikapitiwa na usingizi na kuamka saa mbili usiku. Hicho ndo kilinifanya nichelewe
Mke akaangalia chini na kuona viatu vya mumewe vina mikwaruzo ya nyasi, akafoka na kusema;

Mke: “Muongo mkubwa wa ulikuwa Jimkana unacheza gofu halafu unanidanganya ulikuwa kwa sekretari wako”

USISAHAU SHARE SHARE SHARE SHARE NA MARAFIKI ZAKO facebook ,google+ na twitter

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW: