December 14, 2016

Jaji Mkuu awataka mawakili kuzingatia maadili

JAJI mkuu wa Tanzania Mohamed Othman Chande amewataka mawakili wapya kufanya kazi zao za Uwakili kwa kuzingatia sheria, kanuni na maadili... thumbnail 1 summary
JAJI mkuu wa Tanzania Mohamed Othman Chande amewataka mawakili wapya kufanya kazi zao za Uwakili kwa kuzingatia sheria, kanuni na maadili ya taaluma yao.


Aliyasema hayo leo Jijini Dar es Salaam wakati wa Sherehe za 55 ya kuwapokea na kuwaapisha Mawakili wapya 285 iliyofanyika katika viwanja vya karimjee. Maadili ya mawakili ni mienendo ya mawakili wenyewe, kumekuwa na baadhi ya malalamiko kuhusu kutokutetea mteja kwa kiwango cha sheria kinachohitajika” alisema Jaji Mkuu.

Aidha, Jaji Mkuu amewataka mawakili hao kufuata taratibu za kila wakili kuwa na leseni halali katika kazi zao na kuweza kuhuisha leseni hizo pale zinapokwisha muda wake. Kwa mujibu wa Jaji Mkuu amesema mawakili wana wajibu kujiendeleza kitaaluma kwa kujifunza kila wakati masuala ya uwakili ili kuenda na wakati kwani wakili sio mwisho wa taaluma.

Jaji Mkuu Chande alisema mawakili wana wajibu wa kulinda siri ya mazungumzo baina yao wateja na kuhakikisha wanakuwa na wajibu wa kutokwamisha uharakishaji wa kesi kutokana na mfumo wa sasa ambao unahimiza uharakishwaji wa kesi. Kwa upande wake Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju aliwataka mawakili hao kuwa waaminifu kwa wateja wanaowahudumia na kushirikiana na mahakama katika kutoa haki.

Naye Rais wa Chama cha Wanasheria cha TLS alisema kuna baadhi ya changamoto mbalimbali zinazoikabili tasnia ya sheria nchini ili kufanikisha na kuwa taaluma kamili ya uwakili. Idadi ya mawakili walioapishwa leo imepelekea Tanzania kuwa na idadi ya mawakili 6082.

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW:

No comments