May 02, 2015

PETER WA P-SQUARE AFUNGUKIA BIFU LAO

Peter Okoye. PETER na Paul Okoye wamekuwa wakikwaruzana kila mara kiasi cha kuwashangaza watu ila Peter ameamua kuweka wazi kuwa, kugom... thumbnail 1 summary
Peter Okoye.

PETER na Paul Okoye wamekuwa wakikwaruzana kila mara kiasi cha kuwashangaza watu ila Peter ameamua kuweka wazi kuwa, kugombana kwao kusichukuliwe kama kitu cha ajabu kwani nao ni binadamu Akizungunza na mtandao mmoja nchini humo.

P-square.

Peter alisema kuwa kutofautiana kwao ni jambo la kawaida na imekuwa ikitokea hivyo mara nyingi lakini baadaye maisha yanaendelea.“Huwa inatokea kutofautiana kwa hapa na pale kama inavyotokea kwa wengine, tunakwaruzana kisha tunaweka mambo sawa.

Huwa tunazinguana ile mbaya lakini kesho yake tunaenda stejini pamoja na kufanya shoo na hakuna anayejua. “Yaani sisi ni sawa na wanandoa walioishi zaidi ya miaka 20, lazima kuna siku wanatofautiana,” alisema Peter.

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW: