August 27, 2014

PASTOR MYAMBA WA BONGO MOVIE APATA AJALI

Taswira baada ya ajali hiyo. STAA wa filamu za Kibongo, anayepatia zaidi kuigiza kama Mchungaji, Emmanuel Myamba ‘Pastor Myamba’ amepa... thumbnail 1 summary

Taswira baada ya ajali hiyo.
STAA wa filamu za Kibongo, anayepatia zaidi kuigiza kama Mchungaji, Emmanuel Myamba ‘Pastor Myamba’ amepata ajali baada ya gari
lake aina ya Toyota Creasta kugongwa na gari lingine leo mchana katikati ya Boko na Bunju jijini Dar es Salaam.
Katika ajali hiyo, hakuna mtu aliyejeruhiwa zaidi ya magari hayo mawili kuharibika.

Kwa mujibu wa Pastor Myamba, dereva aliyekuwa akiendesha gari lililogonga gari lake alitokomea na kuacha gari lake eneo la tukio baada ya kugundua kuwa ndiye aliyekuwa na makosa.
Magari yote mawili yamevutwa na 'breakdown' kisha kupelekwa kituo cha polisi Tegeta.

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW: