July 02, 2014

Jeshi La Polisi Iringa lakamata watuhumiwa wa Mwanafunzi Aliyechomwa Moto

Mwili wa Daniel Anael Lema, aliyekuwa mwanafunzi wa mwaka wa nne wa shahada ya sheria katika Chuo Kikuu Kishiriki cha Mt. Augustino, Tawi... thumbnail 1 summary
Marehemu Daniel Anael Lema enzi za uhai wake

Mwili wa Daniel Anael Lema, aliyekuwa mwanafunzi wa mwaka wa nne wa shahada ya sheria katika Chuo Kikuu Kishiriki cha Mt. Augustino, Tawi la Iringa (Ruaha University College – RUCO) umeagwa leo na kusafirishwa kuelekea mkoani kwao kilimanjaro kwa mazishi.

Wanafunzi wa chuo hicho na wananchi wa manispaa ya Iringa walioguswa na tukio hilo walijitokeza katika hospitali ya mkoa wa Iringa ambako shughuli ya kuuga mwili huo ilifanyika.
Jeshi  la Polisi mkoani iringa   linawashikilia watu wanne ambao ni walinzi wa duka usalama waliokuwa wakilinda nyumba moja ya kulala wageni iliyopo Kihesa katika manispaa ya Iringa kwa tuhuma  ya kumchoma moto mwanafunzi  huyo.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoani Iringa Ramadhani Mungi alisema tukio hilo lilitokea Juni 24 majira ya saa tisa usiku baada ya wasamaria wema kutoa taarifa polisi kuwa kuna mtu anatembea akiwa anawaka moto.

Marehemu Daniel Anael Lema enzi za uhai wake
Mungi alisema mara baada ya kupata taarifa hiyo   Jeshi la Polisi lilifika katika  eneo hilo  na kumkuta Daniel  Lema (25)  akiwa ameanguka chini huku akiwa amefungwa mikono nyuma.
Kamanda huyo aliwataja  watuhumiwa hao kuwa ni  Mussa Nganga (28), Costa Mgayuka (38), Steven Kalole (24) na Samson Peter (24) wote wakazi wa Kihesa.
“Tulipopata taarifa tulifika eneo hilo kwa haraka na tukamkuta ameanguka chini tulimfungua ile mikono na kumchukuza vizuri tulimkuta akipumua kwa shida ndipo tukamkimbiza hospitali ya rufaa ya mkoa wa Iringa kwa ajili ya kupata matibabu.”alisema Kamanda Mungi.
Jeneza lenye mwili wa marehemu Daniel Lema kabla ya kuagwa.
Jeneza lenye mwili wa marehemu Daniel Lema kabla ya kuagwa.
Alisema kuwa  mwanafunzi huyo alikuwa baa moja inayoitwa Inbox bar inayomilikiwa na Katibu Mkuu wa zamani wa TFF, Frederick Mwakalebela akipata kinywaji huku akiangalia michuano ya mpira wa miguu (kombe la dunia) ambayo inaendelea nchini Brazili.
“Mwanafunzi alikuwa anaangalia michuano hiyo ya mpira wa miguu kwenye baa hiyo na baada ya mpira huo kuisha aliondoka na kuelekea nyumbani kwako Kihesa kabla ya kufika nyumbani eneo hilo kuna nyumba ya kulala wageni iitwayo Glory lodge ambapo pembeni yake kuna grocery moja iitwayo Glory grocery  akaingia hapo akifikiri ipo wazi ili aendeleze kinywaji,” alisema.
Alisema wakati akigonga mlinzi wa nyumba ya kulala wageni Glory lodge  ambae ni mmasai aitwaye Mussa Nganga alimuona na kumuita ndipo kijana akakimbia na baada ya kukimbia alimfukuza na kuwaita wenzake watatu na kumfanyia kitendo kama hicho.”alisema Mungi.
Baada ya kufikishwa Hospitali ya Rufaa ya Iringa, Lema aliendelea na matibabu yake mpaka alipokutwa na mauti jana majira ya saa nane mchana.

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW: