July 27, 2014

Dr Slaa: Sina Mpango wa kugombea Urais 2015

DK. Willbroad Slaa "Sifikirii kuelekeza nguvu zangu kwenye kuwania  urais 2015 wapo watu wengi wenyesifa ktk kundi la UKAWA.Kila kit... thumbnail 1 summary

DK. Willbroad Slaa "Sifikirii kuelekeza nguvu zangu kwenye kuwania 
urais 2015 wapo watu wengi wenyesifa ktk kundi la UKAWA.Kila kitu 
kitafanywa kwa wakati muafaka, kazi iliyopo mbele yangu ni kupigania 
umoja wetu wa UKAWA ili kuleta ushindani wa kweli katika uchaguzi 
2015.Akizungumzia hatua ya UKAWA kususia Bunge Maalumu la Katiba Dk. 
Slaa alisema umoja huo uko sahihi kwani umesimama upande wa wananchi, 
niaheshimu uamuzi wa Viongozi wangu Mh Freeman Mbowe Prof Ibrahim 
Lipumba na James Mbatia.UKAWA imebeba maoni ya wananchi na suala la 
kutengeneza Katiba sio suala la rais, serikali wala chama chochote 
bali ni la wananchi.Serikali ina viongozi vigeugeu kwa sababu ni wao 
ndio waliosaini rasimu ya Katiba mpya, lkn cha ajaabu wao ndio 
wanageuka na kutaka yajadiliwe mambo ambayo hayamo ndani ya rasimu ya 
Tume ya Jaji Joseph Warioba."

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW: