December 12, 2016

Meli yenye malori 600 ya Kiwanda cha Dangote yawasili Mtwara

Mfanyabiashara Alhaji Aliko Dangote jana alipokuwatana na kufanya mazungumzo na Rais Dk Magufuli, Ikulu jijini Dar es Salaam alimthibitishi... thumbnail 1 summary
Mfanyabiashara Alhaji Aliko Dangote jana alipokuwatana na kufanya mazungumzo na Rais Dk Magufuli, Ikulu jijini Dar es Salaam alimthibitishia kuwa hana lengo la kufunga kiwanda chake kama inavyodaiwa badala yake anatafuta fursa nyingine za kuwekeza hapa nchini.

Katika kuthibitisha hilo, Mfanyabiashara huyo alisema jana meli yenye malori mapya 600 kwa ajili ya kusambazia saruji yake itawasili nchini.

Aliongeza kuwa lengo la kufanyabiashara hapa nchini mbali na kutengeneza faida pia ana lengo la kuisaidia serikali ya Tanzania kutengeneza ajira hivyo hana sababu ya kuagiza mali ghafi toka nje ya nchi ambazo zinapatikana nchini.

Baada ya kufanya mazungumzo hayo, meli yenye magari hayo 600 ilitia nanga katika bandari ya Mtwara ambapo ndipo kiwanda cha Saruji cha Dangote kilipo.

Aidha, imeelezwa kuwa wiki ijayo meli nyingine kutoka Korea Kusini yenye malori 451 inatrajiwa kuwasili katika bandari ya mkoani Mtwara.

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW:

No comments