August 16, 2016

Picha: Jaydee, Alikiba, Juma Nature, Snura wapamba tamasha la Serebuka

Lady Jaydee, Alikiba, Snura, Juma Nature ni miongoni mwa wasanii waliotumbuiza mbele ya mamia ya mashabiki wa muziki jijini Dar es Salaam... thumbnail 1 summary
Lady Jaydee, Alikiba, Snura, Juma Nature ni miongoni mwa wasanii waliotumbuiza mbele ya mamia ya mashabiki wa muziki jijini Dar es Salaam, Jumapili hii kwenye tamasha la Serebuka.

Mamia ya wakazi wa Dar es Salaam waliojitokeza kwenye tamasha la Serebuka lililofanyika kwenye viwanja vya Posta, Kijitonyama

Tamasha hilo liliandaliwa na kampuni ya StarTimes na kudhaminiwa na kampuni ya Huawei Tanzania.

Meneja ya Huawei nchini Tanzania, Huxiangyang Jacko akimkabidhi mshindi wa bahati nasibu simu ya Huawei P9 lite

Jide, Stamina na Kiba ndio waliopata shangwe zaidi huku mashabiki walimtaka hitmaker huyo wa ‘Aje’ aendelee kuimba licha ya muda wa kuendelea na tamasha hilo kuwa umekwisha.

Lady Jaydee akitumbuiza kwenye tamasha hilo

Meneja masoko Huaweim Bi Jane Wang akiongea kwenye tamasha hilo

Alikiba akizikonga nyoyo za mashabiki waliokuwa na kiu ya burudani kwenye tamasha hilo


Chura kaachiwa huru: Snura akionesha mauno yanavyokatwa

Mshereheshaji wa shughuli hiyo, Jokate akiteta jambo na Bi Jane Wang

Juma Nature


Tazama picha zaidi za tamasha hilo.






SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW:

No comments