August 15, 2016

MFAHAMU ANAYEIPA MBINU CHADEMA ZA KUITIKISA SERIKALI NA CCM..!!!

Kama Chadema wana mikakati inayoisumbua CCM; inayoisumbua Serikali au inayovisumbua vyama vingine vya siasa, basi kuna mtu nyuma ya pazia... thumbnail 1 summary
Kama Chadema wana mikakati inayoisumbua CCM; inayoisumbua Serikali au inayovisumbua vyama vingine vya siasa, basi kuna mtu nyuma ya pazia anayebuni na kuratibu mipango hiyo. 

Mbinu tofauti zilizotumika wakati wa Uchaguzi Mkuu zilizofanya wapinzani waweke ushindani wa kihistoria, mbinu zinazotumika wakati likitokea sakata lolote bungeni na mkakati uliotangazwa hivi karibuni wa kupambana na kile kinachodaiwa kuwa ni ukandamizaji wa demokrasia na kupinga ukiukwaji wa sheria, ni mambo yanayokifanya chama hicho kiendelee kuwa midomoni mwa wananchi.

Si mwenyekiti Freeman Mbowe, mwanasheria mkuu wa chama hicho, Tundu Lissu wala kiongozi mwingine yeyote anayebuni mipango hiyo peke yake bila ya kumshirikisha ‘mchawi’ huyo.

Ni John Mrema; yule kada aliyekuwa anaendesha mikutano yote ya kampeni za urais za Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) wakati wa Uchaguzi Mkuu mwaka jana. Ndiye mchawi wa mikakati ya Chadema kwa sasa ndani na nje ya Bunge.
Mrema ni kada wa Chadema ambaye alikuwa meneja wa kampeni za urais za Lowassa, ambayo iliundwa na CUF, NCCR-Mageuzi, NLD na chama hicho kikuu cha upinzani nchini.

Ndani ya Chadema, Mrema sasa ni mkurugenzi wa itifaki, mawasiliano, uenezi na mambo ya nje na kabla ya kupewa cheo hicho, alikuwa mkurugenzi wa masuala ya Bunge na Halmashauri.

“Mimi si mchawi, lakini habari za Chadema hazikauki kwenye mitandao na kwenye vyombo vya habari. Nataka muende wenyewe mkafanye utafiti muone jinsi Chadema inavyotawala kwenye mitandao ya kijamii,” alisema Mrema katika mahojiano na Mwananchi yaliyofanyika Ijumaa iliyopita.

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW:

No comments