May 15, 2016

"Maisha Akili Vingine Mbwembwe Tu" – Dogo Janja

Dogo Janja amewataka vijana kujituma katika nafasi zao za kazi ili kukuza vipato vyao huku akidai maisha ni akili vingine ni mbwembwe. ... thumbnail 1 summary
Dogo Janja amewataka vijana kujituma katika nafasi zao za kazi ili kukuza vipato vyao huku akidai maisha ni akili vingine ni mbwembwe.
Akizungumza na Bongo5 Jumamosi hii, Dogo Janja amesema ukiwa na akili na ni mtu wa kujiongeza ni rahisi kutoka kimaisha.
“Maisha yamebadilika sana, ubunifu, ujanja ujanja, watu wajue maisha ni akili vingine mbwembwe,” alisema Dogo Janja.
“Kikubwa ni kujituma sana, vijana wafanye kazi kwa bidii ndiyo maana nikasema maisha ni akili vingine mbwembwe, kwa sababu ukijiongeza tu, kila kitu kinawezekana,” aliongeza Dogo Janja.
Rapa huyo ambaye anafanya vizuri na video yake ya wimbo ‘My Life’, amewataka mashabiki wa muziki wake kubiria kazi mpya hivi karibuni.

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW:

No comments