March 23, 2016

PETR CECH AIBUKA KINARA JAMUHURI YA CZECH

Mlinda mlango wa klabu ya Arsenal, Petr Cech ametangazwa kuwa mchezaji bora wa mwaka wa Jamuhuri ya Czech. thumbnail 1 summary

Mlinda mlango wa klabu ya Arsenal, Petr Cech ametangazwa kuwa mchezaji bora wa mwaka wa Jamuhuri ya Czech.

Cech Mwenye umri wa miaka 33, alichaguliwa na makocha, wachezaji na viongozi wa timu za nchini humo na kufanikiwa kutwaa tuzo hiyo kwa mara ya nane.

Mlinda mlango huyo alitangazwa kuwa bora, kwa

kuwashinda wachezaji wenzake wa timu ya taifa David Lafata anaeitumikia klabu ya Sparta Prague katika nafasi ya ushambuliaji na Vladimir Darida anaecheza nafasi ya kiungo katika klabu ya Hertha Berlin ya nchini Ujerumani.

Cech, ameshaitumikia timu yake ya taifa katika michezo 118 tangu alipoitwa kwa mara ya kwanza mwaka 2002.

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW:

No comments