February 16, 2016

Saa kadhaa kabla ya kuanza kwa mchezo wa PSG Vs Chelsea, hizi ni rekodi muhimu za kufahamu

Mtu wangu wa nguvu hatua ya 16 bora ya michezo ya Ligi ya Mabingwa Ulaya inaendelea kama kawaida usiku wa leo February 16, Usiku huu nd... thumbnail 1 summary

Mtu wangu wa nguvu hatua ya 16 bora ya michezo ya Ligi ya Mabingwa Ulaya inaendelea kama kawaida usiku wa leo February 16, Usiku huu ndio siku ambayo tutashuhudia michezo miwili ya kwanza ya hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, michezo itakayochezwa leo February 16 saa 22:45 kwa saa za Afrika Mashariki, ni mechi kati yaBenfica dhidi ya Zenit St P, na mchezo ambao unatarajiwa kuangaliwa na watu wengi zaidi, mchezo kati ya Paris Saint Germain dhidi ya Chelsea.

Naomba nikusogezee rekodi chache za mchezo kati ya Paris Saint Germain dhidi yaChelsea, huu unatajwa kuwa ndio mchezo ulioteka hisia za mashabiki wengi wa soka kwa usiku wa February 16 na unaaminika utatazamwa na watu wengi zaidi. Rekodi kutoka mtandao wa 11v11.com hizi ndio rekodi za mechi 6 walizokutana PSG dhidi ya Chelsea,kabla ya mchezo wa saba kuchezwa usiku huu.

Rekodi ya Chelsea dhid ya PSG katika mechi 7 kwa mujibu wa 11v11.com

Chelsea inatajwa kushinda mechi 2 kati ya Sita, imepoteza mechi moja, sare mechi tatu, hivyo kwa mujibu wa takwimu za 11v11.com zinaonesha kuibeba Chelsea zaidi, lakini mtandao wa independent.co.uk unaipa nafasi klabu ya Paris Saint Germain kushinda mchezo huo, kutokana na rekodi yao ya sasa ya kutokufungwa hata mechi moja katika mechi zake 34 za mashindano ilizocheza msimu huu.

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW: