November 22, 2014

Wewe ni shabiki wa Arsenal au Man United – hizi hapa sababu 6 kwanini timu yako inaweza kuibuka mshindi leo hii

Leo kwenye ligi kuu ya Uingereza utakapigwa mchezo ambao kwa miaka zaidi ya miaka 15 umekuwa ukivuta hisia za mabilioni ya mashabiki wa sok... thumbnail 1 summary

69a451c0-7101-11e4-8b7c-815175f865ee_ArsenalVsManULeo kwenye ligi kuu ya Uingereza utakapigwa mchezo ambao kwa miaka zaidi ya miaka 15 umekuwa ukivuta hisia za mabilioni ya mashabiki wa soka ulimwenguni kote – Arsenal FC wanaikaribisha Manchester United kwenye uwanja wao wa Emirates.

Kuelekea kwenye mchezo huo millardayo.com inakuletea sababu 6 kwanini mashabiki wa timu hizi mbili wategemee kupata matokeo chanya leo hii.
SABABU 3 KWANINI ARSENAL KESHO WANAWEZA KUPATA MATOKEO MAZURI
The Gunners hawajapoteza mechi hata moja kwenye uwanja wao wa nyumbani msimu huu kwenye ligi kuu ya England, wakiwa wameshinda mara mbili na kutoa sare mara 3 kwenye mechi zao 5 walizocheza Emirates Stadium.
Rekodi ya Manchester United kwenye viwanja vya ugenini ni mbovu mno. wameshindwa kushinda katika mechi zao tano kwenye ligi wanapocheza ugenini msimu huu.
Alexis Sanchez yupo on fire, amefunga magoli sita katika mechi 4 zilizopita za ligi kuu.
SABABU 3 KWANINI MAN UNITED KESHO WANAWEZA KUPATA MATOKEO MAZURI
United hawajapoteza mechi hata moja katika 3 za mwisho walizotembelea uwanja wa Emirates Stadium.
Arsenal hawajaifunga United katika mechi zao sita zilizopita.
United hawajapoteza mechi hata moja katika mechi 18 zilizopita dhidi ya vijana wa Arsenal Wenger.

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW: