December 09, 2016

FAHAMU WATU 10 MASHUHURI DUNIANI WALIOJIBADILI JINSIA YA KIKE NA KUWA WANAUME..!!!

  KATIKA orodha ya watu maarufu duniani ukiachilia mbali wacheza sinema, wanasiasa na wanamuziki, wapo wanaume ambao walipozaliwa mpaka... thumbnail 1 summary
 
KATIKA orodha ya watu maarufu duniani ukiachilia mbali wacheza sinema, wanasiasa na wanamuziki, wapo wanaume ambao walipozaliwa mpaka miaka yao ya mwanzo ya maisha, walikuwa wakijitambulisha kama wanawake kutokana na utata wa kimaumbile, hatimaye wakaamua na kujitambulisha kama wanaume.



Alizaliwa mwaka 1980 na kutambuliwa kama mwanamke na alipewa jina la kike la Yvonne Buschbaum. Alikuwa akishiriki michuano mbalimbali ya kimataifa ya kuruka kwa upondo na nchini kwake Ujerumani alikuwa ni mrukaji bora wa pili wa upondo miongoni mwa wanawake wanaoruka kwa upondo.

Mwaka 1987 alijiuzulu uchezaji wa mchezo huo. Wakati akiwa ameachana na mchezo huo, ndipo alipoamua kujibadilisha rasmi jinsia yake kwa kutumia madawa ya kuongeza vinasaba vya kiume, na hivyo kusaidia kumwelekeza kwenye jinsia ya kiume. 


Mwaka 2008, alibadili rasmi jina lake la kike na kuchukua jina la kiume, sambamba na hilo alifanyiwa upasuaji na kuwa mwanamume kamili.











Huyu ni mtengeneza sinema za kiutu uzima anayechukuliwa kama alama ya uwakilishi wa wasagaji na mashoga. Mwaka 2007, Buck alikuwa mshindi wa kanda za video za kiutu uzima wa mwaka (Adult Video News Award "Transsexual Performer of the Year"). 




Hivi sasa anafanya kazi kama mwanasheria, muelimishaji, mhadhiri na mwandishi anayemiliki kampuni yake ya utengenezaji wa sinema.







Loren Cameron











Loren Rex Cameron ni mpiga picha, mtunzi na mwanaharakati wa watu wanaoishi na jinsia mbili. Ni mtu maarufu miongoni mwa wanaharakati wa jinsia na anazo kazi nyingi alizofanya zenye lengo la kuipatia elimu jamii kuhusiana na masuala ya jinsia ikiwemo wale wenye jinsia mbili.







Ian Harvie






Mmarekani Ian Harvie ni muigizaji wa vichekesho, anayetumia maumbile yake ya jinsia kama chombo kwenye maigizo yake. Ameigiza na waigizaji maarufu akiwemo Margaret Cho na wengineo wengi.




Lucas Silveira












Alizaliwa nchini Canada mwaka 1979, Lucas Silveira aliweka historia kwa kuwa mwanamuziki wa kwanza wa muziki wa rock kujitangaza hadharani kwamba ana jinsia mbili ingawa anajitambulisha kama mwanaume. 




Amekuwa mwanamuziki wa kwanza kupata mkataba wa kurekodi na kampuni kubwa ya kutengeneza muziki. Silveira ni mwimbaji, mpiga gitaa na mtunzi wa nyimbo wa kundi la The Cliks







Katastrophe












Rocco Kayiatos anafahamika kama Katastrophe, ni mwamuziki na mtayarishaji wa muziki wa hiphop nchini Marekani. 




Kayiatos anatajwa kama mwanamuziki wa kwanza wa HipHop kujitangaza hadharani kwamba ana jinsia mbili mongoni mwa wanamuziki wa hip-hop.







Thomas Beatie












Thomas Beatie alijipatia umaarufu duniani kama mwanaume wa kwanza aliyebeba mimba. Akiwa amezaliwa mwanamke, Beatie aliishi maisha yake kama mwanamke mpaka alipofikia umri wa miaka 20. 




Alianza kutumia madawa maalum ya kumwongezea vinasaba vya kiume mwilini mwake, lakini akaamua kuendelea kubaki na sehemu zake za jinsia za kike ili yeye na mkewe ambaye hana uwezo wa kubeba mimba waweze kupata watoto kwa kutumia mbegu za kiume za watu wanaojitolea. 




Beatie tayari amepata watoto watatu na amerudia kutumia madawa ya kumwongezea vinasaba vya kiume.







Ryan Sallans












Jina la kike alilokuwa akilitumia ni Kimberly Ann Sallans, na hivi sasa ni mmoja wa wanaharakati kwa miaka kadhaa na kumalizia zoezi lake hilo mwaka 2005. 




Sallans amewahi kuonekana kwenye kipindi cha "Larry King Live!" na kituo cha televisheni cha LOGO channel, sambamba na kwenye majarida mengine na machapisho kadhaa.




Andreas Krieger











Andreas Krieger alikuwa mrusha tufe aliyekuwa akiwakilisha timu ya taifa ya mchezo Ujerumani Mashariki. Tangu akiwa mtoto wa chini ya miaka kumi alikuwa akipewa vidonge vya kuongeza nguvu (anabolic steroids) bila ya yeye kujua anapewa vidonge hivyo kwa sababu gani, lakini jambo hilo lilimsaidia kuwa mtu mwenye misuli ilyojengeka katika muonekano na tabia. 




Krieger alijiuzulu kutoka kwenye michezo mwaka 1990 na kufanyiwa upasuaji wa kubadili jinsia yake mwaka 1997. Amekuwa akisema hadharani kwamba anatamani asingeingizwa kwenye matumizi ya dawa hizi ili aweze kutambua hali yake hii mwenyewe na kuamua mwenyewe badala ya kulazimishwa kwa madawa.







Chaz Bono











Ni binti wa wanamuziki maarufu na tajiri sana nchini Marekani na duniani, Cher na Sonny Bono na kupewa jina la kike la Chastity Bono.




Akiwa amekulia kwenye familia yenye umaarufu mkubwa, alijitangaza kwamba yeye ni msagaji akiwa na umri wa miaka 25.




Kabla ya kugundua kwamba alikuwa na jinsia ya pili, jinsia ya kiume yenye shinikizo zaidi ndani ya nafsi yake. Chaz alifanyiwa upasuaji wa kubadili jinsia uliochukua miaka miwili, na hivi sasa anaishi kwa furaha akiwa ni mwanaume.

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW:

No comments