May 27, 2016

Risasi zapigwa katikati ya show ya T.I New York Marekani, mmoja auwawa

Rapper T.I ambaye pia aliwahi kuja bongo kwenye FIESTA, alikuwa na show New York Marekani katika show usiku wa May 25 2016 akisindikizwa ... thumbnail 1 summary
Rapper T.I ambaye pia aliwahi kuja bongo kwenye FIESTA, alikuwa na show New York Marekani katika show usiku wa May 25 2016 akisindikizwa na Maino na Uncle Murda ambapo kabla T.I hajapanda kwenye stage, ilisikika milio ya risasi.

Taarifa ya polisi imesema mtu mmoja alifariki kwenye tukio hilo na wengine watatu kujeruhiwa ambapo Rapper Troy Ave amekuwa ni mmoja wa majeruhi baada ya kupatwa na moja ya risasi mguuni.

Mpaka sasa Polisi hawajamdaka yeyote aliehusika na ufyetuaji huo wa risasi na uchunguzi bado unaendelea huku ikisubiriwa kauli ya Rapper T.I kuhusu tukio hilo lililotokea kwenye show yake hiyo, unaweza kutazama hii video fupi hapa chini ya jinsi ilivyotokea.

Gunshots just went off at the T.I concert, never been so scared in my life

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW:

No comments