April 23, 2016

Ukimya Wa Msanii Alikiba Wawatesa Mashabiki Wake Kwenye Mitandao Ya Kijamii

Tupo kwenye ulimwengu ambao mitandao ya kijamii imegeuka kuwa kama chakula ambacho ni lazima ule kila siku. Kwa watu maarufu, mitandao imeg... thumbnail 1 summary
Tupo kwenye ulimwengu ambao mitandao ya kijamii imegeuka kuwa kama chakula ambacho ni lazima ule kila siku. Kwa watu maarufu, mitandao imegeuka kuwa sehemu muhimu kwa wao kuwa karibu na mashabiki wao. 
Mashabiki wanatarajia kuona kila hatua ambayo msanii anaipitia katika shughuli zake za kila siku. Wanataka kuona si tu picha zake akiwa studio akirekodi muziki au jukwaani akitumbuiza, bali pia za maisha binafsi kama vile akiwa na familia au washkaji.
Na kwa mashabiki, msanii wanayempenda akiwa kimya hata kwa siku moja tu, hukosa raha na kila wakati huchungulia kwenye akaunti yake kuangalia nini alichoweka. Kwao ni furaha kuona picha za staa huyo na pindi anapoamua kukaa kimya huwanyima kitu muhimu katika yao. Huo umekuwa ni kama ulevi na unaweza kushangaa kwanini mtu anajiskia hivyo lakini ukweli ni kwamba ‘this is real.’
Mashabiki wa Alikiba wanalalamika kuwa amekuwa kimya sana siku za hivi karibuni. Picha ya mwisho kwenye akaunti yake ya Instagram iliwekwa siku sita zilizopita. Wanahisi hawatetendei haki kwa ukimya wake na kwa sababu post zake ni kitu kinachowapa furaha, wameanza kukosa uvumilivu.
Lakini mashabiki wanapaswa kufahamu kuwa wakati mwingine msanii anaweza asiwe na ‘mood’ ya kushare kila kitu kwenye mitandao ya kijamii. Ni kitu cha muhimu lakini sio lazima na ukiangalia post za nyuma, kama wasanii wengine Kiba amekuwa mstari wa mbele kuwaweka karibu mashabiki wake kwa posts za kikazi na familia.
Na mara nyingi anapokaa kimya kwenye mitandao hiyo haiimanishi kuwa hana mambo anayofanya. Beyonce huamua kukaa kimya hata kwa mwezi mzima bila kuweka chochote Instagram.
Nicki Minaj, Rihanna na wasanii wengi tu wamekuwa wakiamua kukaa kimya kwa sababu maalum. 
Nadhani ni muhimu kuacha kuifanya mitandao ya kijamii iwe kielelezo cha mambo yanayoendelea kwenye maisha yetu. 
Kwasababu kabla ya Instagram, Facebook au Twitter, maisha yalikuwa ya heri tu na mashabiki walizoea kuishi karibu na mastaa wanaowapenda hata kwa kusikiliza tu nyimbo zake.

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW:

No comments