April 18, 2016

TUTEGEMEE KOLABO KATI YAO, AMA YOUNG KILLER KASAJILIWA WCB?.

Well yote kwa yote ni kitu kizuri tunategemea kati yao, na siku zote zikikutana ladha mbili tofauti za muziki huleta utamu wa aina yake. thumbnail 1 summary
Well yote kwa yote ni kitu kizuri tunategemea kati yao, na siku zote zikikutana ladha mbili tofauti za muziki huleta utamu wa aina yake.

Picha aliyoiweka rapa wa Kibongo Young Killer kwenye ukurasa wake wa Instagram, imezua maswali kadhaa ya matumaini miongoni mwa mashabiki wake.

Rapa huyo wa Mwanza amepost picha akiwa na Icon Diamond Plutnumz, na kuipa ‘caption’ iliyoacha wengi njia panda kama kamtembelea tu Diamond ofisini kwake, kuna ngoma ya pamoja kati yao au tayari kasajiliwa kwenye lebo ya WCB inayomilikiwa na Chibu?.

“# Hakuna mtu aliye zaliwa ili aje awe maskini (ndiyo ) unaweza ukawa umezaliwa kwenye familia maskini ila ukweli ni kwamba hujazaliwa ili wew uje kua maskini….hivyo bas ::mafanikio uja kwa wale walio shindwa mara nyingi na wakajaribu tena kwa ujasiri.. (yes) mungu nisaidie yatimie .. with MSAFI@diamondplatnumz” ameandika.

Kitu kingine ni jinsi mashabiki na wanaounda timu mbali mbali za Diamond kuirepost picha hiyo na kumkaribisha Young killer WCB.

Tuendelee kusubiri na tutajua kinagaubaga undani wa ‘fumbo’ hili.

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW:

No comments